CONGRATULATIONS AND WELCOME TO MZUMBE UNIVERSITY
The following applicants have been selected to join various
undergraduate programmes (Degree, Diploma & Certificate) at Mzumbe
University Main Campus and Mbeya Campus College in the 2016/2017
academic year. Candidates are advised to observe all instructions.
<<Click here to view Fifth Batch students selected to join the Mzumbe University all Campuses>>
<<Click here to view Fourth Batch students selected to join the Mzumbe University all Campuses>>
<<Click here to view Third Batch students selected to join the Mzumbe University all Campuses>>
<<Click here to view Second Batch students selected to join the Mzumbe University all Campuses>>
<<Click here to view First Batch students selected to join the Mzumbe University all Campuses>>
<<Modality of transfer of selected undergraduate candidates from other Universities/colleges to Mzumbe University 2016/2017>>
<< Inn Campus Hostels Main Campus >>
<< Off Campus Hostels Main Campus >>
<< First Year HESLB Loan beneficiary students 2016/2017 >>
Wednesday, 16 November 2016
Orodha ya vyuo 26 vilivyofutiwa usajili na NACTE
Baraza
la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limevifungia vyuo vya ufundi 26
kutokana na makosa mbalimbali, ikiwamo kushindwa kuzingatia masharti
yaliyowekwa katika cheti cha usajili wa vyuo hivyo, huku likisimamsisha
utoaji wa programu zilizokuwa zikitolewa katika vyuo 20 ambazo
hazijasajiliwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam, Kaimu Katibu mtendaji wa NACTE,
Dkt. Adolf Rutayuga, alisema kuwa wamekuwa wakifuatilia vyuo vya ufundi
ili kutathmini kama vinafuata viwango vya ubora wa kitaaluma
vilivyowekwa na NACTE katika kutoa mafunzo.
Katibu
huyo amesema kuwa baada ya kufanya uchunguzi huo, wamebaini vyuo 26
vilishindwa kuzingatia masharti yaliyowekwa na NACTE katika cheti cha
usajili, huku vyuo 20 vikitoa mafunzo ambayo hayajathibitishwa chini ya
idara isiyotambulika,wakati vyuo viwili vikiwa na vituo vya
satellite/Kampasi ambavyo navyo havijathibitishwa na chombo husika.
NACTE
ni bodi iliyoanzishwa kisheria chini ya Sheria ya Baraza la Taifa la
Elimu ya Ufundi, kifungu cha 129, kusimamia na kuratibu utoaji wa elimu
ya ufundi na mafunzo nchini Tanzania. Chini ya sheria hiyo, ili kufikia
na kudumisha hali ya mtoa mafunzo, vyuo vyote vinatakiwa viwe
vimesajiliwa, vibali na kuwa mitaala iliyopitishwa na baraza. Vyuo
haviruhusiwi kuanza kutoa kuanza kutoa huduma yoyote ya mafunzo bila
idhini ya baraza.
Hapa chini ni mgwanyo wa vyuo katika makundi matatu na hatua zilizochokuliwa dhidi ya kila kundi
Jedwali 1: Vyuo vya Ufundi vilivyofutiwa usajili
| S/N | CHUO |
| 1 | Institute of Management and Development Studies – Iringa |
| 2 | Green Hill Institute – Mbeya |
| 3 | Institute of Business and Social Studies – Mbeya |
| 4 | Loyal College of Africa – Mbeya |
| 5 | Mbeya Training College – Mbeya |
| 6 | Mbengwenya College of Business and Information Technology –Mbinga |
| 7 | New Focus College – Mbeya |
| 8 | Shukrani International College of Business and Administration – Mbeya |
| 9 | Majority Teachers College – Mbeya |
| 10 | Rukwa College of Health Sciences – Sumbawanga |
| 11 | MAM Institute of Education – Mbeya |
| 12 | Belvedere Business and Technology College – Mwanza |
| 13 | Geita Medical Laboratory Sciences and Nursing Training College – Geita |
| 14 | Global Community College – Geita |
| 15 | Muleba Academy Institute – Muleba |
| 16 | St. Bernard Health Training Institute – Katoro, Geita |
| 17 | Victoria Institute of Tourism and Hotel Management – Mwanza |
| 18 | Gisan Institute of Health Sciences – Mwanza |
| 19 | Dar es Salaam Institute of Business Management – Dar es Salaam |
| 20 | SAMFELIS College of Business Studies – Dar es Salaam |
| 21 | Ellys Institute of Technology – Bunda, Mara |
| 22 | Tanzania Institute of Chartered Secretaries and Administrators – Arusha |
| 23 | Emmanuel Community College – Kibaha |
| 24 | Modern Commercial Institute – Dar es Salaam |
| 25 | Marian College of Law – Dar es Salaam |
Jedwali 2: Vyuo vya Ufundi vinavyotoa mafunzo ambayo hayajathibitishwa
| S/N | CHUO | MAFUNZO |
| 1 | MISO Teachers College – Mafinga | Competence Building Network (CBN) – a Certificate in Early Childhood Education |
| 2 | Tusaale Teachers College – Mafinga | Competence Building Network (CBN) – a Certificate in Early Childhood Education |
| 3 | The St. Joseph’s College Institute of Business and Management (SJCIBM) – Morogoro | |
| 4 | The Golden Training Institute – Dar es Salaam | |
| 5 | Nkrumah Mkoka Teachers College – Kongwa, Dodoma | |
| 6 | National Institute of Agriculture (Chuo cha Kilimo cha Taifa) – Arusha | |
| 7 | Musoma Utalii Training College – Musoma | |
| 8 | Mwanza Polytechnic Institute – Mwanza | |
| 9 | Mwanza Polytechnic Institute – Maswa | |
| 10 | Ruter Institute of Financial Management – Mwanza | |
| 11 | Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Mwanza | |
| 12 | Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Geita | |
| 13 | Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Bukoba | |
| 14 | Singni International Training Institute – Bukoba | |
| 15 | Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Kahama | |
| 16 | Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Simiyu | |
| 17 | Richrise Teachers College – Geita | |
| 18 | Twiga Training Institute – Musoma | |
| 19 | Zoom Polytechnic Institute – Bukoba | |
| 20 | St. Thomas Training College – Shinyanga |
Jedwali 3: Vyuo vya Ufundi vyenye Vituo vya Satellite / Kampasi
| S/N | CHUO |
| 1 | MISO Teachers College – Mafinga |
| 2 | Rungemba Teachers College – Mafinga |
Tuesday, 15 November 2016
DPP amwondolea mashtaka mbunge wa Sumve Mhe Richard Ndassa
Hatimaye
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imemwachia huru
Mbunge wa Sumve (CCM), Richard Ndassa (56) baada ya upande wa Jamhuri
kuomba kumuondolea kesi kushawishi na kuomba rushwa ya Sh.milioni 30.
Ndassa
alikuwa anakabiliwa na shtaka la kushawishi na kuomba rushwa kutoka
kwa Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Felichesmi
Mramba.
Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dennis Lekayo jana aliwasilisha maombi ya kumwondolea Ndassa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa.
Lekayo
alidai kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), ameona hana nia ya
kuendelea na mashtaka yaliyopo mahakamani dhidi ya mshtakiwa chini ya
kifungu cha 98 (a) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA).
Aidha
kwa mujibu wa kifungu hicho kinampa mamlaka DPP ya kumwondolea mashtaka
mtuhumiwa kabla ya kusikiliza ushahidi lakini anaweza kukamatwa na
kushtakiwa upya.
Hakimu
Nongwa alisema kwa kuwa upande wa Jamhuri umeomba kumwondolea mshtakiwa
mashtaka na kwamba hawana nia ya kuendelea na kesi hiyo, mahakama yake
imekubali ombi hilo.
"Mahakama
hii inamwachia mshtakiwa chini ya kifungu cha 98 (a) kama upande wa
Jamhuri ulivyowasilisha maombi yao dhidi ya mshtakiwa" alisema Hakimu
Nongwa.
Mapema
mwaka huu, Mbunge huyo ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya kudumu ya
Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, alifikishwa mahakamani hapo na
kusomewa shtaka la kushawishi na kuomba rushwa ya Sh. milioni 30.
Katika
kesi ya msingi, Lekayo alidai kuwa Machi 13, mwaka huu, jijini Dar es
Salaam, Ndassa aliomba rushwa Sh.milioni 30 kutoka kwa Mramba.
Ilidaiwa
kuwa aliomba rushwa ili awashawishi wajumbe wenzake wa kamati hiyo
watowe mapendekezo mazuri katika mahesabu ya fedha ya Tanesco kwa mwaka
wa fedha 2015/2016.
Katika
shitaka la pili, mwakilishi huyo wa wananchi siku ya tukio la kwanza
pia aliomba rushwa ya huduma ya umeme kwa kumshawishi Mramba atowe
huduma hiyo kwa ndugu wa mbunge huyo Matanga Mbushi,Richard Ndassa na
rafiki wa ndugu yake Lameck Mahewa.
Mbunge huyo alikana mashitaka yake na alikuwa nje kwa dhamana.
Monday, 14 November 2016
MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WADAIWA SUGU - BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU,WALIOMALIZA KATI YA 1994-2014
ORODHA YA WADAIWA SUGU HII HAPA
Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inatangaza orodha ya majina ya
Wadaiwa Sugu ambao wamehitimu katika Vyuo mbalimbali vya Elimu ya Juu
kuanzia mwaka wa masomo 1994/1995. Wasugu hao wanapewa siku 30
kulipa madeni yao ndani ya muda huo kabla hatua za kisheria
hazijachukuliwa na wahusika kulazimika kulipia gharama za kuwasaka na
kuendesha kesi.
Kwa mawasiliano zaidi piga 0763 459 165 au 0767 513 208 au tembelea ofisi zetu za Makao Makuu, Dar es salaam au ofisi zetu za kanda zilizopo Dodoma, Zanzibar, Mwanza na Arusha.
Kuona orodha hiyo bofya viunganishi vifuatavyo:
Kidato cha Pili Waanza Mitihani leo
Wanafunzi
wa kidato cha pili nchini wameanza kufanya mitihani yao ya upimaji leo
katika shule za sekondari 4,669 zilizopo Tanzania Bara.
Jumla ya wanafunzi 435,221 wamesajiliwa kufanya mitihani hiyo wakiwamo 67 wasioona na 306 wenye uoni hafifu.
Mbali
na mitihani hiyo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa
(Necta), Dk Charles Msonde amesema mtihani wa Taifa wa darasa la nne
utafanyika Novemba 23 na 24, mwaka huu.
"Mitihani
hii inafanyika katikati ya mafunzo ili kubaini changamoto zilizopo na
kutafuta namna ya kuboresha mafunzo hayo," amesema Dk
Msonde.
Wakati
huo huo, Dk Msonde amefafanua kuwa mafunzo ya ualimu wa shule ya msingi
ngazi ya stashahada yamefutwa lakini wanafunzi waliopo vyuoni
watamalizia masomo yao kwa muda uliobaki.
Dk Msonde amesema mafunzo hayo ya walimu yataendelea kwa utaratibu wa zamani ambao ulikuwa ngazi ya cheti.
Amesema usimamizi wa mitihani hiyo itakuwa chini ya Necta kama ilivyokuwa zamani badala ya Nacte.
"Wanafunzi
walio vyuoni wataendelea na mafunzo hayo, isipokuwa kuanzia mwaka huu
hatutadahili kwa ngazi ya diploma, tutadahili ngazi ya cheti kama
ilivyokuwa zamani," amesema Dk Msonde.
Mikopo elimu ya juu yapeleka kilio Udom
ZAIDI ya wanafunzi 200 waliodahiliwa katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom)
kwa mwaka (2016/17), wamelazimika kuacha masomo na kurejea nyumbani
baada ya kukosa mikopo ya elimu ya juu kutoka serikalini.
Imeelezwa kuwa wanafunzi hao wa mwaka wa kwanza walifika mapema chuoni
hapo kabla ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kutoa
majina ya wanufaika na wamefikia uamuzi huo baada ya bodi hiyo
’kuwatosa’ kutokana na kukosa sifa za kupata mikopo hiyo.
Aidha, zaidi ya wanafunzi 100 waliokuwa wanaendelea na masomo chuoni
hapo wamelazimika kusitisha kwa muda masomo yao kutokana na kuondolewa
kwenye orodha ya wanufaika kutokana na kubainika kuwa awali waliingizwa
kwenye orodha hiyo pasi na sifa za kupatiwa mikopo.
Saipulani Abubakar, waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo,
aliiambia Nipashe jana kuwa kutokana na kukosa mikopo kutoka HESLB,
wanafunzi hao wameshindwa kujilipia ada na kumudu gharama za maisha ya
chuo na wameamua kurudi nyumbani.
“Nusu ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wameamua kurudi nyumbani kutokana
na kukosa mikopo kutoka serikalini, wengi ni watoto wa maskini,
wameshindwa kujilipia na kuamua kurudi nyumbani kufanya shughuli
zingine,” alisema Abubakar.
Alisema hadi mwishoni mwa wiki, ni wanafunzi wachache waliosajiliwa
chuoni hapo na hawafiki hata nusu ya waliodahiliwa kwa ajili ya mwaka
huu wa masomo.
Aidha, Abubakar alisema wapo wanafunzi wanaosubiri hatma yao kutokana na
HESLB kupeleka majina kwa mafungu katika vipindi tofauti chuoni hapo.
Alisema wanafunzi hao kwa sasa hawakai chuoni na wamekuwa wakiondoka na
kurejea chuoni kujua hatima yao.
Alibainisha kuwa miongoni mwa wanafunzi waliorudi nyumbani, wamo
waliopata asilimia ndogo ya mikopo ukilinganisha na ada wanazotakiwa
kulipa na hawana uwezo wa kumalizia kiasi kilichobaki.
Hata hivyo, kiongozi huyo wa wanafunzi alisema serikali yake iliangalia
vigezo vipya vilivyowekwa na bodi na kubaini kuwa baadhi ya wanafunzi
wanakidhi, lakini hawamo kwenye orodha ya wanufaika wa mikopo hiyo mwaka
huu.
Aliiomba serikali kuangalia upya mustakabali wa wanafunzi hao waliorudi nyumbani kwa kuwa wanapoteza ndoto zao.
“Ni kweli bodi iliweka vigezo vya wanafunzi kupata mikopo, lakini
tunashangaa kuona baadhi ya wanafunzi wenye sifa wanakosa, kuna
wanafunzi walisoma shule za kata, wengine hawana wazazi na wanaishi
vijijini ambako maisha ni magumu na wamenyimwa mikopo,” alisema.
"Wapo baadhi ya wanafunzi waliokosa mikopo hiyo, wakaamua kujilipia ada,
lakini kutokana na ugumu wa maisha hasa kukosa fedha kwa ajili ya
matumizi ya kawaida, wameamua kuahirisha mwaka ili wakajipange kwa ajili
ya mwaka ujao," aliongeza.
NUSU MWAKA
Alisema zaidi ya wanafunzi 100 waliokuwa wakiendelea na masomo lakini
waliokosa na kuamua kujilipia ada ya nusu mwaka, walifika ofisini kwake
kuandika barua za kuahirisha mwaka hadi pale hali ya maisha itavyokaa
vizuri na kuwapa fursa ya kuendelea na masomo.
Alisema kuwa kwa taarifa waliyopewa na HESLB, inaeleza kuwa wanafunzi
walioondolewa kwenye orodha ya wanufaika wa mikopo kwa mwaka huu wa
masomo licha ya awali kupewa, wamebainika kutumia vyeti feki vya vifo,
majina yao kutoonekana kwenye vitivyo wanavyopangwa na kutosaini
uthibitisho wa kupatiwa fedha.
Kiongozi huyo pia alibainisha kuwa kuna wanafunzi wanaondelea na masomo
lakini hawana uhakika kama wataendelea kunufaika na mikopo hiyo kwa kuwa
usajili kwa ajili ya mwaka huu wa masomo umesitishwa kusubiri HESLB
itoe majina ya wanafunzi inaoendelea kuwapa mikopo.
Kutokana na hali hiyo, Abubakar alisema serikali ya wanafunzi chuoni
hapo imeamua kukutana na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Ufundi, Maimuna Tarish na Mkurugenzi wa HESLB, Abdul-
Razaq Badru, Novemba 20, mwaka huu kuzungumzia hatima ya wanafunzi
waliokosa mikopo.
Alipotafutwa na gazeti hili jana, Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu
na Mawasiliano wa HESLB, Cosmas Mwaisobwa, alisema wanafunzi watakaopata
fedha mwaka huu ni wale waliokidhi vigezo vilivyowekwa.
Alisema bodi imefanya uchambuzi yakinifu wa kujua nani anastahili kupata mikopo hiyo na nani hastahili.
Mwaisobwa alisema bodi haiwezi kutoa msaada wowote kwa wanafunzi
waliokosa mikopo na kuamua kurejea nyumbani kwa kuwa kutokana na mfumo
wa kielektroniki uliotumika kufanya uchambuzi, imeweza kubaini wanafunzi
wenye sifa na wasio na sifa.
Mwaisobwa alisema “Sisi tunafuata sifa na vigezo vilivyowekwa vya utoaji
wa mikopo, hata kama wangerudi wote nyumbani, tunachoangalia ni vigezo
vya kupata huo mkopo”.
Alisema mwaka wa masomo 2016/17 Udom ulianza Oktoba 29, mwaka huu na
kwamba baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliobahatika kupata
mikopo, walipewa fedha kwa ajili ya chakula na malazi Ijumaa iliyopita.
Hivi karibuni, HESLB ilitangaza kuwaondoa zaidi ya wanafunzi 3,000
kwenye orodha ya waliotarajiwa kunufaika na mikopo hiyo kwa mwaka huu wa
masomo kutokana na kile ilichokielezwa kuwa ni kupungukiwa sifa.
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru, alisema mbali na
kuondoa wanafunzi hao, wengine 87 ambao awali hawakujumuishwa kwenye
orodha ya wanufaika kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo kusoma shule
zisizo za serikali, sasa watapata mikopo baada ya kubainika walisomeshwa
na wafadhili.
Taarifa iliyotolewa na Badru Oktoba 30, ilibainisha sifa za wanufaika wa
mkopo kuwa ni wanafunzi yatima na walemavu, wanaotoka familia za hali
duni hususani waliosoma shule za umma na wale wanaosoma fani zilizo
kwenye kipaumbele cha taifa.
Fani hizo ni sayansi za tiba na afya, ualimu wa sayansi na hisabati, uhandisi wa viwanda, kilimo, mifugo, mafuta na gesi asilia.
Fani nyingine ni sayansi asili huku ya mwisho ikiwa ni sayansi ya ardhi, usanifu majengo na miundombinu.
Katika mwaka huu wa masomo, upangaji wa mikopo hiyo unazingatia bajeti
ya Sh. bilioni 483 zilizopitishwa na Bunge zikitarajiwa kunufaisha
wanafunzi 119,012, kati yao 25,717 wakiwa ni wa mwaka wa kwanza na
93,295 wanaoendelea na masomo yao.
Vyoo 100 kujengwa barabara ya Mwanza Kwenda Dar Es Salaam
Taasisi
ya The Desk & Chair Foundation (TD& CF), inatarajia kujenga
vyoo 100 katika Barabara Kuu ya Mwanza-Shinyanga-Dar es Salaam
unaokadiriwa kutumia Sh. milioni 500.
Mwenyekiti
wa TD & CF, Alhaji Sibtain Meghjee alisema hivi karibuni mjini
Mwanza kwamba mradi huo ni sehemu ya miradi mitatu mikubwa ambayo
taasisi yake inatekeleza nchini.
Alisema
baada ya kukamilisha mradi mkubwa wa jengo la kupumzikia wananchi
wanaokwenda kutibiwa na kuwajulia hali wagonjwa waliolazwa katika
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure wanatarajia kujenga
vyoo 100 kwenye barabara ya kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam kwa basi.
Meghjee
alieleza kuwa maandalizi ya awali ya mradi huo yameshaanza na kwamba
watashirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu
(SUMATRA) na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) ili kupata taarifa
sahihi kabla ya mradi kuanza.
“Penye
nia pana njia, baada ya kukamilisha ndoto yetu, leo ya mradi huu mkubwa
wa ujenzi wa jengo la kupumzikia hapa Sekou Toure, tunatarajiwa
kutekeleza miradi mitatu mikubwa ukiwemo wa vyoo kwa ajili ya abiria
wanaosafiri kati ya Mwanza na Dar es Salaam:
“Tunataka
msamiati wa kuchimba dawa wakati wa safari ubaki kuwa historia kwa hiyo
tunatarajia kufanya jaribio moja la kujenga matundu 100 ya vyoo katika
njia na barabara kuu ya Mwanza hadi Dar es salaam ambavyo vitagharimu
shilingi milioni 500.Tutashirikiana na mamlaka husika, ofisi yako na
idara ya afya,”alisema Meghjee.
Meghjee
alieleza kuwa taasisi hiyo pia ina mpango wa kutekeleza mradi wa
kutengeneza viungo bandia kwa kushirikiana na kitengo cha Jairpur
Foot/Knee and Limb Project cha India ambao unahitaji Dola 200,000 za
Marekani (sh. milioni 44), zitakazowezesha kuanzisha huduma ya viungo
hivyo bandia vya miguu, mikono, fimbo na baiskeli.
Alisema
wanaendelea kuwasiliana na wafadhili watakaoshirikiana nao kwenye mradi
huo na kuwahakikishia walengwa kuwa viungo hivyo vitapatikana kwa
gharama nafuu mara utakapokamilika mradi huo.
Meghjee
aliongeza kuwa wakati wakiendesha ujenzi wa jengo la mapumziko katika
Hospitali ya Sekou Toure,walipata wazo la kujenga mabanda yatakayotumiwa
na madereva wa pikipiki (boda boda) kuegesha vyombo vyao kivulini na
kupata huduma ya vyoo na mabafu.
Mwenyekiti
huyo wa TD & CF aliongeza zaidi kuwa endapo Halmashauri ya Jiji
itaridhia na kuwapa eneo maalumu na mahususi la ujenzi wa huduma hiyo
watafanya jaribio hilo moja ili kuweza kuona matunda yake.














