Saturday, 5 November 2016

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA CHUO KIKUU ST.JOHN UNIVERSITY -SJUT 2016/2017 6TH ROUND

KUONA MAJINA 
Share:

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA CHUO KIKUU MARIAN UNIVERSITY-MARUCO 5TH ROUND 2016/2017

KUONA MAJINA
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI NOVEMBER 5 2016



Share:

Marekebisho saba Yafanyika Muswada wa sheria ya huduma za habari

Serikali jana imewasilisha bungeni muswada wa sheria ya huduma za habari mwaka 2016, huku ikitaja marekebisho saba katika muswada huo.
Share:

Majibu ya JPM kwa wanahabari kuhusu muswada wa Sheria ya Huduma za Habari 2016


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
Share:

Magufuli: Vyombo Vya Habari Simamieni Kujenga Maadili Na Utamaduni Wa Mtanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli ametoa wito kwa vyombo vya Habari nchini kuwa mbele katika kusimamia Maadili na kuutangaza Utamaduni wa Mtanzania.
Share:

Rais Magufuli Awataka Watanzania Kutumia Fursa Zilizopo

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amewataka watanzania kutumia fursa zilizopo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kwa ajili ya kuliletea maendeleo ya taifa.

Aliyasema hayo jana Jijini Dar es Saalam wakati wa mkutano wake na Wahariri wa vyombo vya habari nchini katika kuadhimisha mwaka mmoja wa Utawala wake, ambapo alisema kuwa ipo haja ya kuzungumza na kuelimisha watanzania juu ya fursa zilizopo katika taasisi hizo.

“Katika Jumuiya hizo zipo fursa nyingi kwa ajili ya maendeleo ingawa inahitajika elimu ya kutosha kwa watanzania kuona fursa zilizopo ikiwemo ufundishaji wa lugha ya Kiswahili nchi za nje” alisema Rais Magufuli.

Mbali na hayo, akizungumza kuhusu suala la kupambana na Rushwa nchini Rais Magufuli alitoa wito kwa vyombo vinavyohusika na kupambana na rushwa kufichua watu wote wanaojihusisha na vitendo hivyo.

Rais Magufuli alisema kuwa vita ya Rushwa ni ya kila mwananchi, ambapo alitoa wito kwa watanzania wote kwa ujumla kujiepisha na masuala ya rushwa kwani rushwa ni kansa ya maendeleo nchini.

“Taifa litakwama tukiacha suala la rushwa liendelee, tumeumia kweli kweli katika hili hivyo nitoe wito kwa watanzania wote kwa ujumla kujiepusha na masuala haya kwa ajili ya maendeleo ya nchi kwani kesi ya rushwa ni yetu sote” alifafanua Rais Magufuli.
Share:

Friday, 4 November 2016

KAULI YA RAIS JPM KUHUSU AJIRA MBALIMBALI TANZANIA

 
 Amesema kwamba;
"Sitambui kama usitishwaji wa ajira bado unaendelea mimi nilisitisha kwa miezi miwili tuu baada ya miezi hiyo kuisha zoezi la kuajiri liliendelea na hata juzi tumeajiri madoctor na tunatarajia kuajiri wengine 5000 keshokutwa..ni maneno ya mkuu wa Nchi alipokuwa na mahojiano leo na wahariri mbalimbali"
 
Share:

Yaliyojiri Kutoka Ikulu: Mahojiano ya Rais John Magufuli na Wahariri wa Vyombo vya Habari


Habari wakuu,
Jana ilikua siku ya 365 tangu ilipotimia November tano mwaka Jana na nchi yetu kubadilisha utawala wake kwa njia ya kura zilizopigwa mwezi October.

November tano akaapishwa Daktari John Pombe Magufuli kuwa Rais wa awamu ya tano akimrithi mtangulizi wake, Rais wa awamu ya nne, Daktari Jakaya Mrisho Kikwete.

Leo Rais Magufuli atafanya mahojiano na waandishi wa vyombo vya habari kuuelezea mwaka wake mmoja madarakani ikiwemo kuulizwa maswali ambayo atayajibu moja kwa moja.

Tuwe sote kwenye kipindi cha masaa mawili tujuzane yatakayojiri kutoka viwanja vya Ikulu.
========

Kinachoendelea kwa sasa ni Rais Magufuli kujitathmini baada ya Tido mhando kutoa maneno ya utangulizi.

Rais Magufuli:
Niwashukuru sana kwa michango yenu mikubwa katika maeneo yenu ya kazi.

=>Amesema anahisi ametimiza malengo kwani makusanyo yameongeza kutoka bilioni 800 mpaka 1.2. Anagusia suala la ndege, anasema haiwezekani kujenga utalii bila ndege za uhakika. Kasema sasa ziko tatu na nyingine itakuja mwezi wa sita, mwisho jumla zitakua saba. Anagusia flyover ya Tazara.

=>Kuhusu kilimo, anasema wawekezaji wameshaanza kuja na wakulima wameshaanza kuona matunda ya kuweka maelekezo mazuri katika kilimo. Anatolea mfano kilimo cha korosho kuwa bai ya korosho imetoka Tshs 1000 mpaka 4000 kwa kilo. Pia Pamba bei imeongezeka.

=>Kuhusu nishati bajeti ya mwaka huu ni trilioni 1.3 na anaongelea mradi wa nishati wa Kinyerezi.

Elimu, bajeti ya elimu mwaka huu 4.47, wakati anaingia bajeti ya elimu bure haikuwepo lakini walitoa extra ya makusanyo kugharamia elimu bure japo ina changamoto zake ikiwemo kuongezeka kwa en 84 26

=>Bajeti kwa ajili ya kuwakopesha wanafunzi imeongezeka kutoka bilioni 340 mpaka 473 na wanafunzi wameongezeka kutoka 98,000 mpaka 124,320. Tulipochukua hatua za kuwakopesha wanafunzi wengi zimejitokeza changamoto ikiwemo wanafunzi hewa, katika maendeleo yoyote changamoto huwa zipo.

=>Mfumuko wa bei umeshuka kutokea asilimia 7 hadi 4.5, watu watauliza hela mbona hazipo na zitaendelea kutokuwepo kwa watu ambao ni wapiga dili.

=>Tuna helium na nchi zenye madini hayo ni tatu tu duniani, pia graphite hivyo nchi hii ni tajiri sana.

=>Kulikuwa na safari za hovyo hovyo za watu kupishana angani na nimeanza mimi, nilialikwa mikutano 47 ila nimeenda 3. Pamoja na kufanya hivyo bado marafiki zetu wametuheshimu na kuja kututembelea.

=>Tumepanga Tanzania kuwa ya viwanda, wawekezaji wapo, kwa maoni yangu ninaona tunaenda vizuri katika kuwatumikia watanzania. Nisije kumaliza maswali, asante sana.

Swali(Tido Mhando): Ulichukua muda kuunda baraza la mawaziri, Je Katika tathmini hiyo wanafanya kazi kulingana na ulichotegemea wakifanye

Jibu(Magufuli): Serikali niliyonda imenisaidia sana na wanafanya kazi zao vizuri, niliona niwe na baraza la watu wachache katika kuwatumikia wananchi, changamoto zipo lakini nina imani kubwa.

Swali(Lulu Sanga TV 1): Kuna changamoto kubwa sana ya dawa, watoto wengi wanakufa kutokana na kukosa dawa, unaoneje ukibana matumizi kupata dawa ukazigawa hospitali kubwa au kampeni kama ile ya madawati.
Jibu(Rais Magufuli): Katika bajeti yetu tumetenga bilioni 1.99 na tumeongeza bajeti ya kununulia madawa karibu mara kumi. Tumebadilisha utaratibu badala ya kununua kutoka kwa suppliers sasa tunanunua moja kwa moja kutoka viwandani pia kuna nchi zinataka kuwekeza kujenga viwanda vya kutengeneza madawa hapahapa.
Swali

Jibu: Katika kazi yoyote Sijakandamiza demokrasia ndio maana unaona bunge linaendelea na chaguzi zinaendelea hata hapa wamechagua UKAWA, demokrasia ina mipaka yake, baada ya uchaguzi lazima watu waendelee na production
Swali(Tido)-Nyongeza: Kuna watu wanasema unataka kuelekea kwenye udikteta
JIBU: Tafsiri kila mmoja ana yake na kila mmoja ana uhuru wa kufukiria anavyofikiria hata wewe Tido ulihama BBC, TBC na sasa uko Azam, mwingine anaweza kufikiri uko ulikokuwa kulikuwa na udikteta wa aina fulani.
Swali(Rioba): Unasisitiza uchumi wa viwanda, Tanzania imeshawahi kuwa na viwanda vikafa, kuna watu wanaona hili swala waachiwe watu binafsi, wewe unaoneje?
Jibu: Ilani inasema tunataka kujenga nchi ya viwanda, huwezi kutegemea serikali katika kujenga viwanda ndio maana nikasema kuna makampuni kutoka Kenya na sio makampuni ya watu binafsi.
Swali(Mtanzania): Serikali imeweka mkazo kwenye kupambana na majangili lakini tishio ni kubwa,
Jibu(Rais Magufuli): Umezungumza ukweli na ni changamoto ila pia ina historia yake, sheria ya mifugo ya mwaka 59 ila tumejipanga kuhakikisha haya masuala yasije yakawa parmanent na tumeibadilisha wizara ya maliasili na nimeteua majenerali kuongoza wizara nadhani umeshajua tunataka kufanya nini. Hatuna viwanda vya nyama nchi hii ndio maana mifugo haina pakwenda.
Swali(Magazeti ya serikali): Ni nini mkakati wa kuwafanya watanzania kuona fursa katika sekta nyingine
Jibu(Rais Magufuli): Sisi kama serikali ni kuwaelimisha waweze kutumia fursa zilizopo katika nchi nyingine, mfano sisi tunasifika kwenye Kiswahili, kila mmoja ajipange badala ya kusubiri serikali. Fursa zipo ikiwemo EAC na SADC ambako Tanzania ni mwanachama. Ni wajibu sisi wa watanzania kuchangamkia fursa.
Swali(Tido Mhando): Ulitilia mkazo Rushwa na ufisadi, mwaka mmoja sasa unasemaje?

Jibu(Rais Magufuli): Matunda yameanza kuonekana, nidhamu kazini imeanza kuonekana, tumepitisha sheria ya mafisadi na kesi ya kwanza imeanza kusikilizwa jana. Rushwa na swala mtambuka na haliwezi kushughulikiwa na Rais peke yake. Nitoe wito kwa watanzania wote tukatae Rushwa, ni kansa ya maendeleo.
Swali(Rioba): Kuna maswala umeyasimamia kwa ujasiri ikiwemo ujangili na dawa za kulevya, nini kinakuumiza kichwa
Jibu(Rais Magufuli): Yanayoniumizwa kichwa ni mengi pamoja na swali lako, yale niyoahidi katika miaka mitano bado sijayamaliza na hayawezi kumalizika ndani ya mwaka mmoja. Kwenda mbele unahitaji support ya watu wengi. Mwenyezi Mungu pamoja na support ya watanzania.
Swali(Tuma-Radio Tumaini): Hongera sana, Kura yangu ilifanya kazi, Walemavu wa chini hali bado ni mbaya, tunazo sheria nyingi tunaishukuru serikali. Mazingira yetu(walemavu) bado ni magumu, tunaomba watu wa chini watu iwaangalie.
Jibu(Rais Magufuli): Nimelipokea ombi lako na tutaendelea kulishughulikia na serikali inajali sana walemavu kwani hata sisi ni walemavu wa kesho, nimeunda wizara maalum ya walemuavu, nimewateua walemavu katika baraza langu ikiwemo Dr Possy, Amon Mpanju.

Swali(Bakari Machumu Mwananchi): Viwanda na utajiri wa madini, umeelezea umuhimu wa PPP, kuna wafanyabiashara wanahisi wanatengwa, upande wa madini, tunaunganisha vipi

Jibu(Rais Magufuli): Wafanyabiashara hawajatengwa na tunawahitaji sana, na mimi nawapenda kweli wafanyabiashara lakini nataka wanaolipa kodi. Mfanyabiashara ambae hajalipa kodi anawaumiza ambao wamelipa kodi, ukishakua na wafabiashara wa aina mbili unawaumiza wanaolipa. Palikuwa na mamabo ya hovyo, sitaki kwenda kwenye detail sana maana mambo mengine yapo mahakamani, wafabiashara matapeli siwapendi.

Jibu(Rais Magufuli): Kuhusu madini, ni kweli nchi hii ina madini mengi sana, madini yanatakiwa kunufaisha nchi hii, siku moja yatakwisha, nina uhakika sasa mambo yataanza kwenda vizuri baada ya kusaini regulations. Sisi tuna mafuta pia, tutaunganisha bomba la hoima kwenda Tanga, Tanzanite inapatikana Tanzania tu lakini nchi iliyoongoza kuuza ni India ikifuatiwa na Kenya. Sasa hivi umeanzishwa mnada hapa. Watu wanasafirisha makontena kwenda nje kusafishwa na sisi wenyewe tunayasindikiza. Kwa nini tusitengeneze hapa, haya ndio ndio najaribu kuyazungumza ili nchi yetu isiendelee kuibiwa, kwenini kila sehemu kwenye madini kuna kiwanja cha ndege, hili sio suala la Rais pekee ili pesa zinazopatikana ziwanufaishe watanzania wote. Unachosema ni sawa na kinachotakiwa sasa kusonga mbele.

Swali(Joseph Kulambwa): Tanzania ya viwanda, serikali imejipangaje kutrain mafundi mchundo kuliko wasimamizi wa viawanda

Jibu(Rais Magufuli): Vyuo vya kati tulivibadilisha kuwa vyuo vikuu, ilikua bad direction ndio maana sasa tunajenga vyuo vya VETA ikiwezekata kila mkoa. Hata chuo cha usafirishaji kimekua chuo kikuu na inawezakana kwa sababu kulikua na mikopo ambayo hairudishwi ndio maana sasa kuna deni la trilioni 3.5.
Swali: Wafanyakazi hewa wameondolewa lakini bado mishahara inayolipwa ni mikubwa?

Jibu(Rais Magufuli):
Siku za nyuma kuna madai mengi ambayo yamepelekea serikali kulipa kiasi cha bilion 22.6 na bado kuna madai 39,000 yenye thamani ya sh bilioni 23
Suala la OC bado halitakuwepo kwani mambo yanaenda vizuri.
Aidha serikali itaendele kulipa madeni ya walimu na wakandarasi wanaodai.

Swali(Angalieni Mpendu): Suala la utamaduni na maadili, umeliwekaji katika utawala wako?

Jibu(Rais Magufuli): Jukumu la ku-maintain utamaduni wetu ni la kila mtanzania, kuna wizara inayoshughulika suala hili. Kila mtanzania ana wajibu wa kutunza utamaduni wetu.
Vyombo vya habari vitoe ushrikiano kwa kuhakikisha utamaduni wetu unakuwa mzuri.

Swali(Bukuku): Serikali ya china na Tanzania ni Marafiki, Unaonaje kam ungefanya mazungumzo ma Wachina kukawa na ushirikiano katika mafunzo na mashine ndogondogo

Jibu(Rais Magufuli): Nimeshazungumza nao, wachina wamekubali na wanataka kuchukua eneo la Bagamoyo wajenge viwanda 1000. Pia tumezungumza na serikali ya India katika suala kama hilo hilo. Tumezungumza na serikali ya Morocco na kutakuwa na ndege ya moja kwa moja kutoka Kasablanca hadi JNIA.
Tumeweka fedha katika benki ya TIB kwa ajili ya kukopesha wajasiriamali. Tatizo ni kwamba watu wanakopa lakini hawarudishi ikiwemo wanasiasa. Tatizo la waandishi wa habari hawaaniki watu hawa.

Swali(Tido Muhando): Mchakato wa katiba Mpya umefikia wapi?

Jibu(Rais Magufuli): Katika kampeni yangu hakuna sehemu ambayo nimezungumzia suala la Katiba Mpya, hata hivyo suala la katiba mpya limefika mahali pazuri lakini niacheni kwanza ninyooshe nchi.
Swali(Edoni Mwanika): Kwa nini miswada ya habari inakuwa haipewi muda wa kutosha kujadiliwa na huletwa kidharura tu?

Jibu(Rais Magufuli): Sheria yeyote ina misingi yake, mchakato wa sheria hizi umeanza mwaka 2010 hadi mwaka huu, hakuna muda sahihi ungetosha kujiandaa.
Hata hivyo hili ni suala ambalo lipo ndani ya maamuzi ya bunge hivyo siwezi kuingilia,
Punde musuada huu utakaponifikia nitaisaini na kama ni marekebisho yatafuta.

Swali(Frank): Umeokoa kiasi gani kwa kutosafiri nje? umechukua hatua gani kuhakikisha ukandaa wa Afrika mashariki unakuwa salama? Suala la diaspora wana

Jibu(): Fedha tulizookoa ni mabilioni, hata hivyo siyo kwamba hatusafiri kabisa ili tunahakikisha kunakuwa na uwakilishi ambao unapunguza gahrama.

Tumekuwa tunashughulikia migogoro inayoendelea, DRC nimemtuma mwenyekiti wa mawaziri kwenda ili kutafuta suluhu. Suala la migogoro linadiliwa mezani, Burundi tumemteua Mh Mkapa na anasuluhisha na mambo yanaenda vizuri.

Swali(Sanga): Una maoni gani katika ishu ya Zanzibar na Utawala bora?
Jibu(Rais Magufuli):
Hali ya Zanzibar wamefanya uchaguzi wao vizuri na Dr shein anafanya vizuri na mambo yanaenda vizuri

Swali(Manyere): Msimamo wetu kuhusu Morocco; Je Ikulu haiwezi kuandaa tuzo kwa waandishi wanaondika mambo mazuri kuhusu nchi?

Jibu(Rais Magufuli): Tanzania ni nchi isiyofungamana na upande wowote na hivyo tuna uhuru wa kushirikiana na nchi yeyote.
Hata hivyo Moroco tunashirikiana na nao katika kukuza biashara

Vyombo vya habari vinafanya kazi nzuri kwelikweli,
Nashirikiana na kila mtu hata Masoud anavyonichora kichwa kimevimba hapa, nashirikiana naye.

Swali(Pasco Mayala): Ulitumia mamlaka gani kuamuru bunge na mahakama kufanya unayoyataka? ulitumia mamlaka gani kuzuia mikuatana ya kisiasa?

Jibu: Serikali ndiyo inahusika na kugawa fedha zote kupitia bajeti, fedha zikitumika vibaya anayehusika ni serikali.

Swali: Ulizungumziaje suala la ajira? Umekuta mambo
Jibu(Rais Magufuli): Ajira zilikuwa hazijazuiliwa, serikali imetoa ajira za madaktari na manesi ya hospitali ya Rweganzira.
Zuio la ajira lilikuwa la muda tuu. Mpaka sasa kuna benki iliyorudisha fedha za wafanyakazi hewa kiasi cha shilingi bilioni 6.7.

Serikali inaajiri kwa uangalifu mkubwa ili kuhakikisha suala la wafanyakazi hewa
Serikali imeajiri zaidi za watumishi 5000 kwenye vyombo mbalimbali.

Serikali inaendelea kuboresha maslahi ya wakulima kwa mfano wa korosho; Kilo ya korosho imeongezeka bei kutoka shilingi 600 hadi sh 4000.

Bado tutapanga muda wa kuonana na kujadili zaidi mambo mbalimbali kwa maslahi ya nchi.
Ninawapenda, nitawasaidia, nipo pamoja na ninyi na ninawapenda.

"Katika kitu nilichokuwa natamani sana ni kuhudhuria fiesta ya kesho kwani ndiyo natimiza mwaka mmoja :D:D"

Mungu awabariki sana

==========














Share:

Mgomo: Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wamekesha usiku wakilalamikia Mikopo november 4 2016

 Image result for udsm.ac.tz
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wamekesha usiku wa kuamkia leo Novemba 4, 2016 ikiwa ni mgomo waliouanza wakilalamikia masuala mbalimbali yanayohusiana na mikopo.
Share:

Serikali ya Mkoa wa DAR kusomesha wanafunzi wa sayansi bure mikoa mingine igeni

Share:

ARDHI UNIVERSITY:Candidates Selected for Undergraduate Admission 2016/17 (Third and Fourth Selection)

Share:

BODI YA MIKOPO:MSAKO WA WADAIWA SUGU KUANZA KARIBUNI

 Image result for HESLB.GO.TZ
Share:

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA AWAMU YA NNE, UHAMISHO NA KUONGEZWA KWA MUDA WA KUFANYA MAOMBI KATIKA KOZI ZA ASTASHAHADA (CHETI) NA STASHAHADA (DIPLOMA) KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017



Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu Waombaji wote walioomba kudahiliwa katika kozi za Astashahada (Cheti) na Stashahada (Diploma) na Umma kwa ujumla kuwa dirisha la maombi lilifungwa mnamo tarehe 15 Oktoba 2016 ili kuruhusu uteuzi wa awamu ya nne kwa waombaji wa kozi hizo.

Uteuzi wa awamu ya nne kwa waombaji wa Astashahada na Stashahada unatarajiwa kutangazwa mnamo tarehe 2 Novemba 2016, hivyo basi waombaji wanaombwa kuwa na subira ili kutoa muda kwa Baraza kukamilisha taratibu za uteuzi huo.
Share:

Walimu Watatu Watiwa Mbaroni Kwa Kuwazuia Wanafunzi Kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne


POLISI mkoani Dodoma inawashikilia walimu watatu wa shule za sekondari kwa tuhuma ya kuwazuia wanafunzi wa kidato cha nne, kufanya Mtihani wa Taifa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema kwamba walimu hao wa shule za sekondari za Zoissa na Mnyakongo wilayani Kongwa, walikamatwa Novemba Mosi mwaka huu.

Kamanda Mambosasa alisema kwamba, wakati wa mtihani wa somo la Kiingereza, walimu hao walimzuia mwanafunzi Amina Said wa shule ya sekondari Zoissa kwa madai ya kuwa ni mjamzito na kumpeleka kituo cha afya, kupimwa muda wa mtihani, lakini majibu yalionesha hakuwa na ujauzito.

Aidha, mwanafunzi Bahati Ntigonza wa shule ya sekondari Mnyakongo, alizuiliwa kuingia katika chumba cha mtihani kwa kuwa hakuvaa sare ya viatu, hivyo alirudishwa nyumbani kuvaa viatu huku wenzake wakiendelea na mtihani.

Kamanda Mambosasa aliwataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Lukonge Mwezo ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Mnyakongo, Omari Athumani Mkuu wa Shule ya Sekondari Zoissa na Daud Suleimani John aliyekuwa mwalimu wa zamu katika shule ya sekondari Mnyakongo.
Share:

Magazeti ya Leo Ijumaa ya Novemba 4 2016


Share:

Thursday, 3 November 2016

Arusha: Mwanafunzi wa Chuo cha Tumaini, Makumira abakwa hadi mauti



Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza chuo tajwa abakwa adi kufariki dunia na habari kutoka kwa wanafunzi hapo wadai watu takribani 30 wamekamatwa. 
 
NOTE: Picha zinazoonesha Mwili wa Marehemu, zimeondolewa.

Hapa chini ni Picha wakati wa uhai wake.
Screenshot from 2016-11-02 20-08-40.png 11149393_720637041378317_2234484587156489954_n.jpg 10366004_833474033427950_9208513346806462691_n.jpg
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger