Thursday, 30 June 2016
Polisi Yaua Majambazi Matatu Yaliyokuwa Yamejificha Katika Mapango ya Amboni
POLISI
mkoani Tanga imewaua watu watatu katika mapigano ya risasi wanaodaiwa
kuhusika katika mauaji ya watu jijini humo wakiwamo watu wanane
waliochinjwa katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima.
Limewahakikishia
wananchi kwamba eneo la Amboni yakiwemo Mapango ya Majimoto yanayodaiwa
kutumiwa na wahalifu waliosababisha mauaji hasa ya wakazi wanane wa
Kibatini lipo salama, baada ya watuhumiwa wengine watatu na silaha
mbalimbali kukamatwa juzi.
Waliokamatwa
ni Abdulkarim Singano, Seif Jumanne na Ramadhani Mohamed ambao baadaye
walikufa kutokana na majeraha ya risasi wakati wa mapigano katika msitu
wa Kibatini wakati askari wakijaribu kuwadhibiti, siku moja baada ya
Abuu Seif anayedaiwa kuwa kiongozi wao kuuawa jijini Dar es Salaam.
Silaha
zilizokamatwa ni bunduki mbili aina ya SMG, bastola moja, risasi 30,
mapanga, majambia ambavyo vimepatikana kupitia msako ulioshirikisha
kikosi kazi cha vyombo vya ulinzi na usalama vilivyohusisha askari
kutoka majeshi yote.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo alibainisha hayo wakati akitoa
taarifa ofisini kwake jana kwamba, wahalifu hao walikamatwa Juni 28,
mwaka huu wakati askari walipokuwa katika harakati za kuwakamata kwenye
msitu wa Kibatini jirani na mapango ya Majimoto, Kata ya Mzizima jijini
Tanga.
“Majambazi
waliohusika kuua wananchi wanane pale Kibatini ndio tumewakamata lakini
kwa bahati mbaya watatu kati yao wamekufa wakati wakidhibitiwa na
askari,” alisema Kamanda Paulo.
Alisisitiza wameyakagua yaliyokuwa maficho yao na kujiridhisha kuwa Amboni iko salama na imedhibitiwa.
Alisisitiza wameyakagua yaliyokuwa maficho yao na kujiridhisha kuwa Amboni iko salama na imedhibitiwa.
Mapema
wiki hii, Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, walitangaza kumuua
Abuu Seif aliyeshiriki katika mauaji ya Tanga, baada ya kumpiga risasi
alipokataa kujisalimisha baada ya kubainika kujificha katika nyumba moja
jijini Dar es Salaam. Alifariki dunia akipelekwa hospitali.
Wednesday, 29 June 2016
VIDEO:TUNDU LISSU AWEKWA RUMANDE,HII HAPA VIDEO ALIYOMUITA RAIS JPM DIKTETA UCHWARA
June 28 2016 Mbunge wa Singida
Mashariki, Tundu Lissu alifikishwa Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kwa
ajili ya kujibu tuhuma za uchochezi kupitia gazeti la mawio kwenye
habari yenye kichwa kinachosema ‘Zanzibar Machafuko yaja’ dhidi yake na wenzake watatu.
Nje ya mahakama hiyo Lissu alizungumza na waandishi wa habari ambapo
alitoa kauli ambayo imewafanya polisi wamuite kwa ajili ya mahojiano,
Lissu alisema….>>>’nchi yetu inaingizwa kwenye giza nene na dikteta uchwara hatuwezi kuongozwa na mtu wa namna hiyo, hata kama kachaguliwa na kuwa Rais‘
Lissu
alifika kituo kikuu cha polisi Dar es salaam kuitikia wito wa polisi
na amehojiwa na polisi kwa masaa matatu kutokana na kauli hiyo atalala
rumande leo kwa amri ya ZCO baada ya kukosa dhamana na atafikishwa
mahakamani kesho.
VIDEO HII HAPA
BREAKING NEWS: WANAFUNZI 10 CHUO CHA BUGANDO WAFUKUZWA CHUO,BAADA YA KUKIUKA SHERIA ZA MITIHANI
Habari zilizotufikia ni kwamba wanafunzi 10 wa chuo cha Bugando wamefukuzwa chuo kutokana na kukamatwa wakiibia kwenye chumba cha mtihani.
SOMA BARU HII HAPO CHINI;
SOMA BARU HII HAPO CHINI;
UHAMISHO FORM 5 2016:SERIKALI YAPIGA MARUFUKU
SERIKALI imesema shule zote zenye nafasi za wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano mwaka huu, zimejaa hivyo hakuna nafasi ya mwanafunzi kubadilishiwa shule au mchepuo aliochagua.
Hayo yalibanishwa jana katika taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya
habari mjini hapa na Msemaji wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (Tamisemi), Rebecca Kwandu.
Kwandu alisema baada
ya serikali kutangaza wanafunzi waliojiunga na kidato cha tano, baadhi
ya wazazi na wanafunzi wamekuwa wakifika ofisi za Tamisemi kuomba
kubadilishiwa shule au tahasusi (michepuo) walizochaguliwa.
“Tunapenda
kuwaarifu kwamba shule zote zenye nafasi za wanafunzi wa kujiunga na
kidato cha tano mwaka 2016 zimejaza, hivyo hakuna kinachoweza
kubadilishwa,” alisema Kwandu.
Aidha, Kwandu alisema vigezo
ambavyo vilitumika katika uchaguzi huo ni pamoja na ufaulu na uchaguzi
wa wanafunzi wenyewe juu ya masomo wanayopenda kuendelea nayo kidato cha
tano na sita.
“Kulingana na utaratibu uliowekwa na serikali,
mwanafunzi mwenye sifa za kuchaguliwa kuendelea kidato cha tano na vyuo
vya ufundi ni yule ambaye ufaulu wake ni kuanzia daraja la kwanza hadi
la tatu. Wanafunzi hao wamepangwa kulingana na ufaulu wao masomo
waliyochagua na nafasi zilizopo,” alisisitiza.
Pia alisema nafasi
za shule walizopangiwa wanafunzi zimezingatia miundombinu ya shule
husika na uwezo, na kwamba kila shule imepewa wanafunzi kulingana na
nafasi zilizopo, hivyo hakutakuwa na nafasi ya kuwabadilisha kutoka
shule moja kwenda nyingine kwa sasa.
Kutokana na hali hiyo,
aliwataka wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na
vyuo vya ufundi kuripoti katika shule na vyuo walivyopangiwa kama
walivyoelekezwa.
Alisema mwanafunzi ambaye hataripoti ifikapo
Julai 24, ambayo ni tarehe ya mwisho kwa muda uliopangwa, atakuwa
amepoteza nafasi yake kwa kuwa itachukuliwa na mwanafunzi mwingine
ambaye hakupata nafasi awali.
AJALI YA BASI:WATU WATANO WAFARIKI ,13 WAJERUHIWA JIJINI MWANZA
WATU watano wamefariki dunia na wengine 13 kujeruhiwa katika ajali ya basi lenye namba za usajili T. 449 BCB mali ya kampuni ya Super Sami lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mwanza.Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamikia leo katika eneo la Bashini Kata ya Mabuki Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, baada ya gari hilo kugonga jiwe lililokuwa barabarani na kusababisha William Elias, Dereva wa gari hilo kushindwa kulimdu.Watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni Valieth Odede, William Elias (Dereva) huku mwanaume mmoja na wanawake wawili wenye umri wa miaka 25- 30 majina yao bado yakiwa bado hayajafahamika mpaka hivi sasa.
Majeruhi katika ajali hiyo ni 13, ambao ni Sophia Miraji, Kibilo Mwacha, Boniphace Charles na Frank Kunyumi ambao wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya awali kutokana na kujeruhiwa vibaya.
Wengine ni Stanley Zacharia, Sia Dauson, Hellen Leheke, Michael Leonard, Kudra Ibrahim (mtoto wa miaka miwili), Zamda Issa, Marieth Christopher, Elizabeth Simon na Dickson Msamba ambao wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC) jijini hapa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, akizungumzia tukio hilo, amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari hilo kuwa katika mwendo kasi na kusababisha ashindwe kulimdu basi hilo na kusababisha kupinduka.
Msangi, amesema kuwa kutokana na ajali hiyo jeshi la Polisi mkoani hapa linaendelea kuchunguza gari hilo pamoja na kufanya uchunguzi juu ya ajali hiyo iliosababisha vifo vya watu watano kupoteza maisha na wengine 13 kujeruhiwa.