Thursday, 23 June 2016

Magazeti ya Leo Alhamisi ya June 23 , 2016


Share:

Wednesday, 22 June 2016

Sheria ya Mtandao Yanasa Mwingine..Huyu Kamtukana Rais Magufuli kwenye WhatsApp


Sheria ya Makosa ya Kimtandao inaendelea kushika kasi, mwingine tena aingia matatani baada ya kubainika kutumia Lugha mbaya dhidi ya Rais kwenye mtandao wa WhatsApp.


Leonard Mulokozi Kyaruzi anakabiliwa na kesi baada ya kuandika maneno ya kumtukana Rais John Pombe Magufuli si kwenye Facebook kama Isaac Abubakar wa Arusha, bali ni kwenye WhatsApp – Yes ulidhani kwenye magroup unaweza kutukana unavyotaka?


Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyotolewa Jumanne hii, Kyaruzi anadaiwa kutoa kauli hiyo ya kejeli kwenye WhatsApp June 2. 
Aliandika: Hivi huyu Pombe ni kwamba hana washauri? Hashauriki? Au ni zuzu? Bwege sana huyu jamaa, he doesn’t consider the law in place before opening his mouth!. Au na yeye anaumwa ugonjwa wa Mnyika?”
 
Share:

Afande Sele-"Wasanii Hawana Ubunifu Wana Kiki Tu"


Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Afande Sele amesema zamani walikuwa wanatumia rushwa na kujuana ili kuweza kupata air time, lakini sasa wasanii wanatumia skendo ili kujitangaza katika kazi zao.


"Watu wamekosa ubunifu kwenye kazi zao, ile atahari ambayo tulikuwa tunaiona siku za nyuma sasa hivi ndio inajidhihirisha zaidi, watu walikuwa wanapata air time kwa ajili ya rushwa, kujuana, lakini walikuwa hawana ubunifu, kwa hiyo sasa hivi wameamua kutumia kiki za mambo ya mapenzi mapenzi, kwa vile tayari uwezo wao wa kubuni na kusababisha watu wawakubali moja kwa moja kupitia kazi zao unakuwa hakuna" alisema Afande Sele.

Afande Sele amesema kitendo hicho sio kizuri kisipodhibitiwa, kwani kinachangia kwa kiasi kikubwa kuua muziki wa bongo fleva, kwani watu wameshindwa kabisa kuandika mashairi mazuri yenye ujumbe.

"Mtu anakuwa hana uwezo wa kuonyesha uwezo wa kipaji chake moja kwa moja ili kazi zake zisikike lazima atafute namna nyingine ya kusikika na kuonekana, na ndio hiyo kamchukua fulani, mara kazaa na fulani, mara anataka kumuoa fulani, watu wameshindwa kutunga, wameshindwa kushawishi watu", alisema Afande Sele.
Share:

Babu Wa Miaka 65 Ambaka Mtoto wa Dada Yake na Kumpa Ujauzito Huko Kilimanjaro




Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamtafuta mzee wa umri wa miaka 65 Dominick Kweka wa kijiji cha Kisereni wilayani Hai kwa tuhuma za kumbaka msichana wa miaka 16 ambaye ni mtoto wa dada yake (Mjomba) na kumpa ujauzito ambao sasa una umri wa miezi sita. 
 
Akizungumza  kwa njia ya simu kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Bw Wilbrod Mutafungwa amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kuwa juhudi za kumsaka zinaendelea ili afikishwe katika vyombo vya sheria. 
 

Bw Mutafungwa amesema, jeshi la polisi katika mkoa huo halitavumilia kuona vitendo vya ubakaji vikiendelea kutokea kwa watu wa aina hiyo ambao wanakatisha maandalizi ya maisha bora ya wanafunzi wasichana. 
 

Msichana huyo ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Nkuu amesema, mjomba wake huyo alimbaka nyumbani kwake wakati alimpopelekea sola kwa ajili ya kuichaji ili apate nafasi nzuri ya kujisomea nyakati za usiku na ameiomba serikali aendelee na masomo baada ya kujifungua. 
 

Baba mzazi wa msichana huyo Bw Kilasauko Nyuki ameiomba serikali imchukulie hatua kali za kisheria mzee huyo mwenye makazi katika kijiji hicho na majiji ya Arusha na Dar es Salaam ambaye inadaiwa ametoroka baada ya tukio hilo.
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti yua Leo Jumatano ya June 22

Share:

Tuesday, 21 June 2016

New Video | Isha Mashauzi - Jiamini | Download Mp4



Share:

Rais Magufuli amteua Dkt. Jim Yonazi kuwa Mkurugenzi Mtendaji TSN.

 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Jim James Yonazi kuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais Magufuli amefanya uteuzi huo kuanzia tarehe 18 Juni, 2016.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Jim James Yonazi alikuwa Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maarifa katika Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

Dkt. Jim James Yonazi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Gabriel Nderumaki ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
   
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
21 Juni, 2016
Share:

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO VYA HABARI


ut6TAREHE 20/06/2016 MAJIRA YA SAA 07:30HRS KATIKA MSITU WA BUHINDI ULIOPO KIJIJI CHA MAJENGO KATA YA IRENZA TARAFA BUCHOSA WILAYA YA SENGEREMA MKOA WA MWANZA, MARIAM MATHIAS MIAKA [35] MKAZI WA KIJIJI CHA NYANGALAMILA ALIKUTWA AKIWA AMEKUFA KIFO CHA MASHAKA KATIKA MSITU TAJWA HAPO JUU HUKU UCHUNGUZI WA AWALI UKIONYESHA MWILI WAKE UKIWA NA MIKWARUZO KWENYE BEGA LA KULIA PAMOJA NA SHINGO.AIDHA INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIONDOKA NYUMBANI KWAKE SIKU YA IJUMAA YA TAREHE 17.06.2016 MAJIRA YA ASUBUHI NA KWENDA KATIKA MSITU TAJWA HAPO JUU KUTAFUTA KUNI NA NDIPO MAUTI YALIPO MKUTA HUKO, HADI TAREHE 20.06.2016 MAJIRA YA SAA 07:30HRS AMBAPO MWILI WAKE ULIWEZA KUOKOTWA KATIKA MSITU HUO.

JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA MUME WA MAREHEMU AITWAYE PONYIWA JEREMIA MIAKA [37], MKAZI WA NYANGALAMILA KWA MAHOJIANO ZAIDI DHIDI YA TUKIO HILO KWANI ALISHINDWA KUTOA TAARIFA POLISI NA KWA MAJIRANI ANAOISHI NAO KWA KIPINDI CHOTE AMBACHO MKEWE HAKUONEKANA NYUMBANI KWAKE HIVYO KUPELEKEA KUTILIWA SHAKA KATIKA TUKIO HILO.
CHANZO CHA KIFO HICHO BADO HAKIJAJULIKANA, JESHI LA POLISI BADO LINAENDELEA NA UCHUNGUZI PAMOJA NA UPELELEZI KUHUSIANA NA TUKIO HILO, MWILI WA MAREHEMU TAYARI UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI NA KUKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI AKIWATAKA WAONGEZE USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI WAKATI WOTE PANAPOTOKEA JAMBO AU TATIZO WASISITE KUTAARIFU ILI KUWAZA KUZUI VIFO VINAVYOWEZA KUEPUKIKA.
KATIKA TUKIO LA PILI
KWAMBA TAREHE 20.06.2016 MAJIRA YA SAA 13:20HRS NA KUENDELEA KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA WILAYA YA ILEMELA MKOANI MWANZA, ASKARI WALIFANYA DORIA PAMOJA NA MISAKO KATIKA MITAA MBALIMBALI YA WILAYA TAJWA HAPO JUU NA KUFANIKIWA KUWAKATA WATU WA NNE WAKITUHUMIWA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA BHANGI PAMOJA NA POMBE AINA YA GONGO KITENDO AMBACHO NI UVUNJWAJI WA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI
WATUHUMIWA WALIOKAMATWA 1.JANETH MASOLE MIAKA [30], MKAZI WA KISEKE ALIYEKAMATWA AKIWA NA BHANGI MISOKOTO 83, 2. SUZANA DOTTO MIAKA [50], MKAZI WA IGOMBE ALIYEKAMTWA AKIWA NA POMBE YA GONGO LITA 60, 3. MADURU MATHIAS MIAKA [35], MKAZI WA IGOMBE ALIYEKAMATWA AKIWA NA MTAMBO MMOJA WA KUTENGENEZEA POMBE YA GONGO NA, 4. BUSHESHE FAIDA MIAKA [20], PIA MKAZI WA IGOMBE ALIYEKAMATWA NA BHANGI MISOKOTO MIWILI KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI.
AIDHA WATUHUMIWA WOTE WA NNE WAPO CHINI YA ULINZI WA JESHI LA POLISI HUKU MAHOJIANO DHIDI YA TUHUMA ZA UHALIFU WANAOJIHUSISHA NAO YAKIENDELEA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI KUJIBU TUHUMA ZA UHALIFU ZINAZO WAKABILI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI ANAWATAKA WANANCHI WAENDELEE KUTULIA LAKINI WAKIENDELEA KUTO USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLSI ILI LIWEZE KUFANYA KAZI VIZURI NA KUTOKOMEZA UHALIFU WA AINA ZOTE KATIKA MKOA WA MWANZA.
IMESAINIWA NA:
SACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
Share:

TCU:TANGAZO KWA UMMA JUU YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

Share:

HAYA HAPA MAJINA YOTE YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA VETA 2016

Share:

Nape: CCM Imejaa Majipu


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema ndani ya chama hicho tawala kuna majipu mengi yanayohitaji kutumbuliwa. 

Kwa mujibu wa katibu huyo wa uenezi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi, hatua hiyo ndiyo njia pekee ya kuleta mapinduzi na mageuzi ndani ya chama hicho. 
Amesema chama hicho kilishaingiliwa na makolokolo, hivyo yanahitaji kusafishwa yote kwa mustakabali wake. 
Kauli ya Nape ni sawa na ile iliyowahi kutolewa na viongozi wakuu wa nchi. Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan mwanzoni mwa mwaka huu akiwa mkoani Tanga alisema ndani ya CCM kuna watu majipu ambao wameficha makucha ili wasijulikane uovu wao. 
Siku ambayo Rais John Magufuli alipewa cheti na Tume ya Uchaguzi (NEC) baada ya kushinda uchaguzi alikwenda kwenye ofisi ndogo za CCM Lumumba na kuhutubia huku akisisitiza kuwa ndani ya chama hicho kuna watu wanafiki. 
Nape anasema pamoja na kutumbua majipu, chama hicho pia kinahitaji kujitathimini muundo wake kwa kuwa uliopo sasa ni mkubwa na hauendani na hali halisi ya kipato cha chama.
“Muundo wetu ni mzigo mzito unaongeza urasimu. Kwa mfano wajumbe wa NEC hivi sasa wapo zaidi ya 400 ni mzigo mkubwa kwa chama matokeo yake walitumia fursa kutafuta ubunge, inahitaji marekebisho makubwa kwa kuwa uchumi wa chama ni mdogo kwa sasa, tunategemea ruzuku tu. "- Nape
Alisema hata katika upande wa watumishi wa chama wapo wengi sana na wote si wanasiasa, robo tu ndiyo wanasiasa.

Kwa mujibu wa Nape, kwa sasa kinachohitajika ni kutengeneza chama kidogo ili gharama ya kuendesha iwe ndogo. 
Alisema sababu nyingine ya kusafisha chama kutokana na urasimu uliopo; “Lazima tupunguze mlolongo wa vikao vya kutoa maamuzi lakini pia tuangalie upya sera na taratibu zetu.” 
 Akizungumzia watu wenye tabia ya kuhama vyama kama ilivyotokea kwa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa na kundi lake, Nape alisema yeye si muumini wa hilo.

“Mimi siamini katika kuhama  vyama ni sawa na kumsilimisha Papa. Kwangu kuchukua watu kutoka upinzani ni sawa na gari zima kuwekewa vifaa chakavu. Watanzania waliopo katika vyama vya siasa hawazidi milioni 10 kwa nini tunyang’anyane wakati kuna zaidi ya watu milioni 45."- Nape

Akizungumzia utendaji wa Rais John Magufuli, Katibu huyo wa uenezi wa chama hicho anayetarajia kustaafu hivi karibuni katika mkutano mkuu alisema ameanza vizuri na kwamba mtindo wake wa kutumbua majipu ndiyo hasa ulikuwa ufanyike baada ya wananchi kukosa imani na Serikali kwa muda mrefu.
 “Yanayotekelezwa hivi sasa na Rais Magufuli ni ripoti yetu. Baada ya kuzunguka nchi nzima tuligundua mambo mengi na ili kukiweka salama chama hatuna budi kuhakikisha tunasafisha uozo wote. 

“Ilifika wakati wawekezaji wamechukua ardhi hawaitumii, wananchi hawana ardhi tena matokeo yake ni migogoro kila kukicha, walimu wanadai haki yao watu wenye mamlaka hawatimizi wajibu wao matokeo yake kukaanza kujengeka hisia kwamba walimu ni wapinzani.

 "Hivi mtu anakuwaje mpinzani kama anadai haki yake? Mlipe kwanza haki yake uone kama ataendelea na malalamiko,” alisisitiza Nape ambaye aliingia rasmi katika siasa akiwa kijana mdogo wa miaka 20 tu. 
Alisema Rais Magufuli amerejesha heshima kwani nchi ilifika mahali ambapo wezi wa mali ya umma walionekana ndiyo wajanja na wale ambao walikuwa wana maadili walionekana legelege. 
Alisema jamii ilipotea na Taifa lilikuwa likijenga jamii ya ajabu ya watu mafisadi, wezi na wasioogopa mali ya umma na hawakuwa na wa kuwazuia kufanya wanavyotaka. 
 Akizungumzia mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya chama chake uliofanyika mkoani Dodoma mwishoni mwa mwaka jana Nape alisema vikao vilikuwa vya moto sana. 
“Wakati mwingine tulikaa katika mkutano mpaka saa tisa usiku na hata mkitoka hamtazamani usoni kila mmoja anaingia katika gari na kuondoka, palichemka sana.” 
Hata hivyo, Nape alisema anashukuru Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Jakaya Kikwete kwa kuwa na kifua na hiyo ndiyo siri ya kufanikisha mchakato huo. 
Alisema Kikwete ni mtoto wa CCM hivyo ilikuwa rahisi kumkata yeyote kwani uzoefu wake ndani ya chama ulisaidia na kwamba itachukua muda mrefu kupata kiongozi kama yeye lakini pia hawawezi kupuuza kazi iliyofanywa na Katibu Mkuu wa chama hicho Abdulrahman Kinana. 
“Ukongwe ulituvusha lakini pia wazee wakarekebisha mambo tukavuka salama, hali ilikuwa mbaya lakini ndiyo demokrasia,” alisisitiza Nape ambaye ni mtoto wa mwanasiasa mkongwe, marehemu Moses Nnauye. CCM itafanya mkutano mkuu Julai 23 mwaka huu.
Share:

Wataalamu wa Prescion Air na TCAA Waelekea Zanziba r Kuchunguza Tukio la Ndege Kuwaka Moto


Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), wakishirikiana na mafundi wa Kampuni ya Ndege ya Prescion Air wameelekea Zanzibar kuchunguza tukio la ndege ya kampuni hiyo kupata hitilafu na kuwaka moto na kusitisha safari.

Tukio hilo lilitokea Juni 16 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Karume mjini Zanzibar. 

Taarifa iliyotolewa jana na Mkuu wa Mawasiliano wa Prescion Air, Azda Mkullo inasema wamepeleka injini mbadala kwa ajili ya kufungwa.

Inaongeza kuwa baada ya tukio hilo ilimlazimu rubani kuchukua hatua za kuuzima moto na kuirudisha ndege kwenye eneo la maegesho. 

Ndege hiyo wakati ikipata hitilafu ilikuwa imefanya safari zake kati ya Kilimanjaro na Dar es Salaam.Ndege hiyo PW432 ilikuwa na abiria 34 na wahudumu wanne wote walitoka salama.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger