JK: WAFADHILI WAMEIPA
KISOGO SEKTA YA MAJI
TANZANIA imefanikiwa katika sekta mbalimbali kutokana na misaada kutoka
Benki ya Dunia, lakini haijafanikiwa katika sekta ya maji kutokana na
sekta hiyo kutopewa kipaumbele na wafadhili.
Hayo yalisemwa jana na Rais Jakaya Kikwete wakati wa uzinduzi wa
chapisho kuhusu Maadhimisho ya Miaka 50 ya Ushirikiano kati ya Tanzania
na Benki ya Dunia.
Alisema ushirikiano wa Tanzania na Benki ya Dunia, umefanya kazi kwa
miaka 50 ambayo ni ya mafanikio, lakini maji bado yamekuwa changamoto
katika maeneo mbalimbali ikiwemo vijijini na mijini.
Aliongeza kuwa ni vyema wafadhili ikiwemo benki ya dunia kusaidia sekta
ya maji kutokana na maji kuwa hitaji muhimu na kubwa.
Alisema wananchi wengi wamekuwa wakihangaika na kuacha kufanya mambo ya
maendeleo matokeo yake wanahangaikia maji, hivyo ni vyema sekta ya maji
isaidiwe.
“Ukosefu wa maji unasababisha mambo mengi yakiwemo magonjwa na kama
jamii itakosa maji basi magonjwa mengi yataibuka ikiwemo vichocho,
wanawake wengi wanateseka kutokana na kutafuta maji umbali mrefu,”
alisema Kikwete.
Pia alisema kwa upande wa sekta ya kilimo Tanzania imeweza kufanikiwa
japo bado kuna changamoto ya sehemu za kuhifadhia mazao pamoja na uhaba
wa masoko.
“Na imani mtaendelea kushirikiana nasi kwa upande wa masoko ili uchumi
wetu uzidi kukua yapo mengi ya kufanya lakini haya yakifanikiwa tutafika
mbali,” aliongeza Kikwete.
Aliongeza kuwa Tanzania imeendelea na kupambana na rushwa kwani mpaka
sasa rushwa imedhibitiwa kwa kiasi kikubwa huku lengo likiwa ni kufikia
asilimia sifuri.
Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Afrika Makhtar Diop
alisema, ni furaha kuona ubia kati ya benki ya dunia na Tanzania
umefikia miaka 50 ambayo ni miaka ya mafanikio kwa pande zote mbili.
Alisema unapozungumzia miaka 50 ya Benki ya Dunia ni vyema kutambua
mchango wa Rais wa Awamu ya Kwanza Mwalimu Julius Nyerere kwani alikuwa
na uhusiano wa karibu sana na Mc Namara wote wakiwa na dhamira ya pamoja
ya kukidhi mahitaji ya msingi ya kila mtanzania.
“Baada ya kukaribia kuanguka kabisa kwa uchumi wa Tanzania miaka ya 80
Tanzania iliamua kuanza kutumia zaidi mbinu zenye mtazamo wa soko nah ii
ndio ilianzisha ubia kati ya Tanzania na Taasisi ya Benki ya Dunia,”
alisema Diop.
Alisema kupitia miaka 1980 na 1990 benki ya dunia iliweza kusaidia
Tanzania kufufua uchumi na kuwa wa wazi zaidi na nguzo ya uchumi imara.
Rudi Garcia's side have an option to turn the
Colombian forward's loan move from Cagliari into a permanent transfer
for a further £5.7 million after he impressed there last season
Roma have confirmed the loan signing of Victor Ibarbo from Cagliari for a €5 million (£3.6m) fee.
The Colombia forward spent the latter part of last season with the Giallorossi, for whom he made 11 appearances after a initial battle with injury. Ibarbo
has now sealed a further one-year deal with the Italian
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY WATU
watatu wamekufa katika matukio matatu tofauti katika Wilaya za Tarime
na Rorya akiwemo mtu aliyeuawa wakati wanagombania mwanamke.
Kiteto. Chama cha Mapinduzi
(CCM), Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara imezidi kupata pigo baada ya
Mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi wa wenyeviti wa vitongoji 16 vya
mji mdogo wa Mirerani, kwa maelezo kuwa ulikiuka sheria na utaratibu wa
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Hii ni mara ya pili katika kipindi
cha mwezi mmoja kwa Mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi huo ambao
uliwaweka madarakani makada wa CCM.
Wagombea 38 kati ya 42 wanaoomba kuteuliwa na CCM kugombea
Urais,wamerejesha fomu hadi saa 10:30 jioni julai 2,2015.Kati ya hao
Wagombea wanne waeshindwa kurejesha fomu.
KING wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
ametengeneza kichwa cha habari nchini Nigeria baada ya kufunguka kuwa
anampenda ‘vibaya’ staa wa filamu nchini humo, Omotola Jalade Ekeinde,
Ijumaa lina stori kamili.
...