JK: WAFADHILI WAMEIPA
KISOGO SEKTA YA MAJI
TANZANIA imefanikiwa katika sekta mbalimbali kutokana na misaada kutoka
Benki ya Dunia, lakini haijafanikiwa katika sekta ya maji kutokana na
sekta hiyo kutopewa kipaumbele na wafadhili.
Hayo yalisemwa jana na Rais Jakaya Kikwete wakati wa uzinduzi wa
chapisho kuhusu Maadhimisho ya Miaka 50 ya Ushirikiano kati ya Tanzania
na Benki ya Dunia.
Alisema ushirikiano wa Tanzania na Benki ya Dunia, umefanya kazi kwa
miaka 50 ambayo ni ya mafanikio, lakini maji bado yamekuwa changamoto
katika maeneo mbalimbali ikiwemo vijijini na mijini.
Aliongeza kuwa ni vyema wafadhili ikiwemo benki ya dunia kusaidia sekta
ya maji kutokana na maji kuwa hitaji muhimu na kubwa.
Alisema wananchi wengi wamekuwa wakihangaika na kuacha kufanya mambo ya
maendeleo matokeo yake wanahangaikia maji, hivyo ni vyema sekta ya maji
isaidiwe.
“Ukosefu wa maji unasababisha mambo mengi yakiwemo magonjwa na kama
jamii itakosa maji basi magonjwa mengi yataibuka ikiwemo vichocho,
wanawake wengi wanateseka kutokana na kutafuta maji umbali mrefu,”
alisema Kikwete.
Pia alisema kwa upande wa sekta ya kilimo Tanzania imeweza kufanikiwa
japo bado kuna changamoto ya sehemu za kuhifadhia mazao pamoja na uhaba
wa masoko.
“Na imani mtaendelea kushirikiana nasi kwa upande wa masoko ili uchumi
wetu uzidi kukua yapo mengi ya kufanya lakini haya yakifanikiwa tutafika
mbali,” aliongeza Kikwete.
Aliongeza kuwa Tanzania imeendelea na kupambana na rushwa kwani mpaka
sasa rushwa imedhibitiwa kwa kiasi kikubwa huku lengo likiwa ni kufikia
asilimia sifuri.
Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Afrika Makhtar Diop
alisema, ni furaha kuona ubia kati ya benki ya dunia na Tanzania
umefikia miaka 50 ambayo ni miaka ya mafanikio kwa pande zote mbili.
Alisema unapozungumzia miaka 50 ya Benki ya Dunia ni vyema kutambua
mchango wa Rais wa Awamu ya Kwanza Mwalimu Julius Nyerere kwani alikuwa
na uhusiano wa karibu sana na Mc Namara wote wakiwa na dhamira ya pamoja
ya kukidhi mahitaji ya msingi ya kila mtanzania.
“Baada ya kukaribia kuanguka kabisa kwa uchumi wa Tanzania miaka ya 80
Tanzania iliamua kuanza kutumia zaidi mbinu zenye mtazamo wa soko nah ii
ndio ilianzisha ubia kati ya Tanzania na Taasisi ya Benki ya Dunia,”
alisema Diop.
Alisema kupitia miaka 1980 na 1990 benki ya dunia iliweza kusaidia
Tanzania kufufua uchumi na kuwa wa wazi zaidi na nguzo ya uchumi imara.
Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ
Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ
TANZANIA imefanikiwa katika sekta
mbalimbali kutokana na misaada kutoka Benki ya Dunia, lakini
haijafanikiwa katika sekta ya maji kutokana na sekta hiyo kutopewa
kipaumbele na wafadhili.
Hayo yalisemwa jana na Rais Jakaya
Kikwete wakati wa uzinduzi wa chapisho kuhusu Maadhimisho ya Miaka 50 ya
Ushirikiano kati ya Tanzania na Benki ya Dunia.
Alisema ushirikiano wa Tanzania na Benki
ya Dunia, umefanya kazi kwa miaka 50 ambayo ni ya mafanikio, lakini
maji bado yamekuwa changamoto katika maeneo mbalimbali ikiwemo vijijini
na mijini.
Aliongeza kuwa ni vyema wafadhili ikiwemo benki ya dunia kusaidia sekta ya maji kutokana na maji kuwa hitaji muhimu na kubwa.
Alisema wananchi wengi wamekuwa
wakihangaika na kuacha kufanya mambo ya maendeleo matokeo yake
wanahangaikia maji, hivyo ni vyema sekta ya maji isaidiwe.
“Ukosefu wa maji unasababisha mambo
mengi yakiwemo magonjwa na kama jamii itakosa maji basi magonjwa mengi
yataibuka ikiwemo vichocho, wanawake wengi wanateseka kutokana na
kutafuta maji umbali mrefu,” alisema Kikwete.
Pia alisema kwa upande wa sekta ya
kilimo Tanzania imeweza kufanikiwa japo bado kuna changamoto ya sehemu
za kuhifadhia mazao pamoja na uhaba wa masoko.
“Na imani mtaendelea kushirikiana nasi
kwa upande wa masoko ili uchumi wetu uzidi kukua yapo mengi ya kufanya
lakini haya yakifanikiwa tutafika mbali,” aliongeza Kikwete.
Aliongeza kuwa Tanzania imeendelea na
kupambana na rushwa kwani mpaka sasa rushwa imedhibitiwa kwa kiasi
kikubwa huku lengo likiwa ni kufikia asilimia sifuri.
Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Benki
ya Dunia Afrika Makhtar Diop alisema, ni furaha kuona ubia kati ya benki
ya dunia na Tanzania umefikia miaka 50 ambayo ni miaka ya mafanikio kwa
pande zote mbili.
Alisema unapozungumzia miaka 50 ya Benki
ya Dunia ni vyema kutambua mchango wa Rais wa Awamu ya Kwanza Mwalimu
Julius Nyerere kwani alikuwa na uhusiano wa karibu sana na Mc Namara
wote wakiwa na dhamira ya pamoja ya kukidhi mahitaji ya msingi ya kila
mtanzania.
“Baada ya kukaribia kuanguka kabisa kwa
uchumi wa Tanzania miaka ya 80 Tanzania iliamua kuanza kutumia zaidi
mbinu zenye mtazamo wa soko nah ii ndio ilianzisha ubia kati ya Tanzania
na Taasisi ya Benki ya Dunia,” alisema Diop.
Alisema kupitia miaka 1980 na 1990 benki
ya dunia iliweza kusaidia Tanzania kufufua uchumi na kuwa wa wazi zaidi
na nguzo ya uchumi imara.
0 comments:
Post a Comment