Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya ili kuboresha utendaji kazi. Mabadiliko hayo yamezingatia kuwepo kwa nafasi wazi ishirini na saba (27) zilizotokana na:
- Kufariki dunia Wakuu wa Wilaya 3
- Kupandishwa cheo Wakuu wa Wilaya 5 kuwa Wakuu wa Mikoa
- Kupangiwa majukumu mengine Wakuu wa Wilaya 7; na
- Kutengua uteuzi wa Wakuu wa Wilaya 12