Tuesday, 30 April 2024

WATETEZI KABILIANENI NA MBINU CHAFU ZA UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU - OLENGURUMWA


Mratibu wa kitaifa wa Shirika la watetezi wa haki za binadamu Onesmo Olengurumwa akifungua mafunzo hayo

Na Christina Cosmas, Morogoro

WATETEZI wa haki za binadamu wamesisitizwa kuhakikisha wanapata elimu za mara kwa mara ili kukabiliana na changamoto za mbinu chafu za mikakati ya ukiukwaji wa haki za binadamu ikiwemo wizi wa kimtandao.

Mratibu wa kitaifa wa kutoka shirika la watetezi wa haki za binadamu (THRDC) Onesmo Olengurumwa amesema hayo wakati wakitoa mafunzo ya watetezi wa haki za binadamu kutoka maeneo ya nje ya miji kwenye kanda tatu nchini kupitia mtandao wa haki za binadamu.

“Zipo mbinu mpya mbalimbali ambazo wahalifu wanazitumia kwa njia ya mtandao za kukiuka haki za binadamu, mtetezi nae lazima afahamu ni namna gani anaweza kushughulikia na kufuatilia ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanyika ili kuendana na kazi ya mhalifu au mkiukaji wa haki za binadamu anayokwenda nayo” anasema Olengurumwa.

Aidha anasema watoto wamekuwa wakibakwa na watu mbalimbali wakiwemo watu wao wa karibu au viongozi wa dini kwa njia na mbinu mbalimbali ikiwemo kuwalaghai kwa kuwanunulia zawadi na mengine ambayo mtetezi wa haki za binadamu akijua itamsaidia kufuatilia masuala hayo ya ukiukwaji na kuweza kuwa mtetezi mzuri.

Naye Mwanasheria kutoka kituo cha wasaidizi wa kisheria Morogoro (MPLC) Rachel Siwiti alisema wakiwa watetezi wa haki za binadamu kwa wanawake na Watoto tayari wameshafikia asilimia 70 ya kutoa elimu kwa jamii licha ya kwamba bado haina mwamko wa kupokea elimu na kuondoa changamoto hizo.

Siwiti aliishukuru THRDC kwa kuendelea kuwapa mafunzo yatakayowaimarisha kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo wanawake kuonewa kwa kutopata haki zao kama vile mirathi na mkoa kuwa na ndoa nyingi za utotoni.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE APRILI 30,2024



Magazeti
Share:

Monday, 29 April 2024

UWEKEZAJI KWENYE MIUNDOMBINU YA UHIFADHI WA MAZAO UNAENDELEA


Wizara ya Kilimo imeendelea na mikakati kabambe ya uwekezaji kwenye miundombinu ya uhifadhi wa mazao ili kuhakikisha nafaka na mazao mbalimbali yanakidhi vigezo vya ubora katika soko na yanakidhi vigezo vya ubora vya Kimataifa.

Uimarishaji wa miundombinu hii inasaidia kuhakikishia nchi Usalama wa Chakula na kudhibiti magonjwa kama Sumukuvu kwani miundombinu hii huwezesha nafaka kuhifadhiwa kwa muda mrefu bila kuathiri ubora wake.

Pia uwekezaji wa miundombinu ya uhifadhi husaidia kulinda ubora wa nafaka ili kumsaidia mkulima kupata bei nzuri na yenye ushindani katika masoko ya ndani na nje ya nchi



Share:

TRA YAHAMASISHA WAENDESHA BODABODA KULIPA KODI





Na Mbuke Shilagi Bukoba

Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imewataka wafanyabiashara wa bodaboda kulipa kodi kwa mwaka Tsh. 65,000/= ambapo kodi ya TRA inalipwa kwa awamu nne sawa na Tsh. 16200/= kwa miezi mitatu.

Akizungumza katika kikao cha mafunzo ya elimu ya kodi na waandishi wa habari Aprili 25,2024 katika ukumbi wa mkutano wa ofisi ya meneja TRA Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera Meneja wa TRA Mkoa wa Kagera Bw. Castro Johm amesema kuwa kupitia mabadiliko ya sheria ya mwezi Julai 2023 wafanyabiashara wote wa bodaboda wanatakiwa kulipa kodi.

Aidha,  John amesema kuwa wafanyabiashara wote wa bodaboda ambao hawajafanyiwa makadirio waende ofisi za TRA kufanyiwa makadilio na kwamba kutolipa kodi ni kinyume na sheria na kuna penalti ambayo inaweza kuwakumba na kwamba ambaye atakuwa anahitaji ufafanuzi au ana mkwamo wowote afike ili kutatuliwa changamoto yake.

 Kodi yoyote unapolipa mapato unapata stika ya mapato ambayo unaenda kubandika kwenye chombo chako kulingana na umelipa ya mwaka  au miezi mitatu unapata kulingana na stika na kunasitika zinazotofautisha kama umelipa au hujalipa'', amesema.

Sambamba na hayo Bw. John ametoa wito kwa watu wote walio uza au kuuziwa chombo cha moto kufika ofisini ili kubadilisha jina na kwamba utaratibu ni rahisi ambapo ataenda na mkataba pamoja na EFD LIST ili kubadilisha uhamisho wa chombo hicho.

Kama mnavyojua kutobadilisha umiliki kunamadhara mengi kwamfano kumekuwa na kesi chombo cha moto kinatumika kwenye matukio ya uhalifu mfano chombo cha moto kinajina la Castro pengine itajulikana wewe umefanya uhalifu  lakini unakuta uliuza muda mrefu kwahiyo kubadilisha jina mbali na kuwa na uhalali nacho ila pia inakuepusha na mambo kama hayo'', amesema Bw. John
Share:

Sunday, 28 April 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRILI 29, 2024

Magazeti


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger