Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Mh. Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika ukumbi wa Lina's uliopo kata ya Bilele Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Mh. Abdulrahman Kinana katika ukumbi wa Lina's Bukoba
Na Mbuke Shilagi Kagera.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Mh. Abdulrahman Kinana amewakingia kifua wakulima wa zao la Kahawa na Vanila Mkoani Kagera na kutaka walipwe fedha zao kwa wakati.
Ameyasema hayo Jana Septemba 2,2022 katika ziara yeke mkoani humo wakati akizungumza na wananchi katika ukumbi wa Lina's uliopo kata ya Bilele Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.
Amesema kuwa Wakulima wanapouza mazao yao wapewe fedha na sio makaratasi wala mikopo.
"Mtu anachukua Kahawa yako anakupa karatasi mimi sijaja hapa kwa karatasi mimi nimekuja na rupia nakupa Kahawa wewe unanipa Fedha" Amesema Mh. Kinana.
Ameongeza kuwa atafurahi kuona Wakulima wanalima mazao yao na kuwauzia watu binafsi wenye kuweza kulipa kwa wakati ili kuepusha usumbufu wanaokutana nao katika mashirika.
Sambamba na hayo ameongeza kuwa atatafuta soko la vanila katika nchi ya China kwani nchi hiyo inanunua na ina uhitaji wa zao la Vanila hivyo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Albert Chalamila atamuunganisha na aliyepo ubalozini China ili kutafuta masoko huko.
0 comments:
Post a Comment