Leo Julai 5, 2021 Kampuni namba moja ya Huduma za Kidigitali hapa nchini Tigo kwa kushirikiana na wabia Wake ambao ni kampuni ya Simu ya SAMSUNG wametangaza ujio wao mpya uliojaa Ofa tele hasa katika msimu huu wa Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba).
Akitangaza habari hizo njema kwa Wateja wa Tigo na watumiaji wa simu za Samsung,Meneja Mawasiliano Kutoka Kampuni ya Tigo Bi. Woinde Shisael amesema kuwa msimu huu Kampuni ya Tigo Na Samsung wameamua kuja kitofauti lengo ikiwa ni Kujenga uzoefu wa utumiaji wa simu janja hapa Nchini.
"Sasa mtumiaji wa simu za @samsungtanzania anayetaka kuibadilisha simu yake ya zamani aina za Galaxy (S series, Note, A80) kwa kuwa ameitumia muda mrefu au kioo kimeharibika lakini ameshindwa kupata nyingine kutokana na uwezo wa kifedha, anaweza kubadilishiwa simu hiyo na kupewa simu nyingine Kwa punguzo la bei la hadi Tsh 500,000."
Woinde Shisael - Meneja mawasiliano Tigo.
"Tunatambua kwamba watu wetu wanatumia simu mda mrefu Na wanahitaji kuzibadilisha lakini pia wapo wale ambao simu zao zimeharibika vioo, sasa Leo habari njema ni kwamba Ushirikiano huu wa Tigo na Samsung unakwambia kama una moja Kati ya haya mawili usijali, kama una simu ya zamani ambayo unahitaji kuibadilisha njoo katika maduka yetu ya TIGO au Samsung Tanzania peleka simu yako ya zamani na utapewa punguzo la hadi Laki Tano Na sabini na Tano ili uweze kubadilisha simu yako ya zamani Na upewe toleo jipya, Vilevile wateja wetu wanaonunua simu kwenye maduka ya Tigo na Samsung Halafu simu zao zikapasuka / kuharibika kioo waje kwenye maduka yetu ya Tigo na Samsung ili kubadilishiwa kwa gharama ndogo kabisa ya Fundi, Hii ni moja ya Ofa kibao tulizonazo msimu huu wa sabasaba" Alisema Shisael.
UNAWATHAMINI! "Tunaamini ofa hii itawasadia wateja wetu kuwa na simu za kisasa na zenye kioo chenye muonekano mzuri...Ununuapo simu hizi hakikisha unasajiliwa ili uwe na nafasi ya kupata ofa hizi." Suleiman Mohamed - Meneja Samsung Tanzania.
Kwa upande Wake Meneja wa Samsung Tanzania Bwana Suleiman Mohamed amesisitiza wateja wa Samsung hapa nchini kuhakikisha wanajisajili Ndani ya siku thelathini ili waweze kupata ofa hii ya kubadilishiwa kioo kitakapoharibika Ndani ya miezi 12 baada ya kuinunua bila kusahau ile Waranti ya Miezi 24, ambapo kwa sasa mtu atapata ofa ya GB 96 pale atakaponunua simu kwenye maduka ya Tigo au Samsung.
KIOO BUREE: "Pia mteja atayenunua simu za @samsungtanzania kuanzia toleo la #Samsung_galaxy_A32 kwenda juu, ikitokea kioo cha simu yake kimevunjika ndani ya siku 30 baada ya kuinunua, ataweza kutengenezewa Kwa bei nafuu ya Tsh. 140,000 huku akipewa kioo kipya buree kabisa."
Suleiman Mohamed - Meneja wa Samsung Tanzania.
Kwa Maelezo zaidi Tafadhali tembelea kurasa za kijamii za Tigo Na Samsung.
0 comments:
Post a Comment