Wakazi wa kijiji cha Kampi Samaki katika Kaunti ya Baringo nchini Kenya wamepata mshangao baada ya kushuhudia nyoka mkubwa akitoa heshima za mwisho kwa mmiliki wake aliyejulikana kwa jina la William Ewoi aliyefariki dunia siku ya Alhamis Julai 8,2021.
Inaelezwa kuwa siku mbili baada ya mazishi ya mwanaume huyo anayedaiwa kuwa Mganga wa Jadi, nyoka huyo alijitokeza katika nyumba ya marehemu kisha kuzunguka kaburi la marehemu ikiwa ni ishara ya kutoa heshima zake za mwisho.
0 comments:
Post a Comment