Sunday, 11 July 2021

MWENGE WA UHURU WAMULIKA MIRADI YA UKWELI WILAYA YA SHINYANGA…LUTENI MWAMBASHI ATIA NENO

...

 


Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Modest Mkude, kushoto, akimkabidhi Mwenge wa uhuru Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, tayari kwa kukimbizwa wilayani humo.

Na Marco Maduhu, Shinyanga

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Luteni Josephine Mwambashi, ameweka mawe ya msingi na kuona miradi mbalimbali ya maendeleo Wilaya ya Shinyanga (Manispaa ya Shinyanga na wilaya ya Shinyanga), ambapo ameridhishwa na miradi hiyo na hakuna ambao ameukataa.

Zoezi la Mbio maalum za Mwenge wa Uhuru kitaifa wilayani Shinyanga limefanyika leo Jumapili Julai 11,2021 mara baada ya Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Modest Mkude, kuukabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko katika viwanja wa michezo Shule ya Sekondari Mwalukwa wilayani humo.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi yote sita Luteni Mwambashi amesema ameridhishwa na miradi hiyo ambayo imeendana na thamani ya fedha (Value for Money), huku kukiwa na salio la fedha kwenye baadhi ya miradi, na kuagiza ile ambayo haijakamilika kujengwa ikamilishwe haraka ili ianze kutoa huduma.

“Nimekagua miradi yote iko vizuri, na nimeweka jiwe la msingi, na ile ambayo nimetoa maelekezo yafanyiwe kazi, pamoja na kuikamilisha ile ambayo bado ipo kwenye hatua ya ujenzi ili itoe huduma haraka kwa wananchi,”amesema Luteni Mwambashi.

Pia amewapongeza wananchi wa Bushushu kwa kujitoa kuchangia ujenzi wa Zahanati, ambayo itawasaidia kuondokana na adha ya kufuata huduma za matibabu umbari mrefu.

Akitoa ujumbe wa Mwenge wa Uhuru mwaka 2021, amewataka Watanzania, kudumisha amani, kuendeleza mapambano ya Rushwa, madawa ya kulevya, virusi vya Ukimwi, Malaria, kuzingatia lishe bora kwa watoto, pamoja na Halmashauri kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato kwa njia ya kieletroniki.

Kwa upande wao Wabunge wa Shinyanga, akiwamo Mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum, Patrobas Katambi Jimbo la Shinyanga mjini, pamoja na Christina Mzava wa viti maalum, kwa nyakati tofauti waliahidi kuendelea kuwaletea maendeleo wananchi, pamoja na kukamilisha maboma yaliyosalia kujengwa.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akisoma taarifa ya mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, amesema umekimbizwa Kilomita 136, pamoja na kukagua miradi sita yenye gharama ya Sh. milioni 855.

Ameitaja miradi hiyo kuwa ni, Ujenzi Maabara ya Sayansi katika shule ya Sekondari Mwalukwa, Zahanati ya Bushusu, Nyumba nne za watumishi, Jengo la Uthibiti ubora wa shule Kanda ya Magharibi, chumba cha Tehama katika Shule ya Sekondari uhuru, pamoja na kuona maendeleo ya mradi wa maji Ziwa Victoria Masekelo.

Katika hatua nyingine Mboneko amewashukuru wananchi wa Shinyanga, kujitokeza kwa wingi kwenye mbio hizo za Mwenge wa uhuru, huku akiwataka kuendelea kushirikiana na Serikali kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo.

Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2021 inasema “Tehama ni msingi wa Taifa endelevu, Itumike kwa usahihi na uwajibikaji"

Tazama Picha hapa chini.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Modest Mkude, kushoto, akimkabidhi Mwenge wa uhuru Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, Tayari kwa kukimbizwa wilayani humo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiushika Mwenge wa Uhuru tayari kwa kukimbizwa wilayani humo leo.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, akiushika Mwenge wa Uhuru.
Mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum, akiushika Mwenge wa Uhuru.
Mbunge wa Vitimaalum mkoani Shinyanga Christina Mzava, akiushika Mwenge wa Uhuru.
Mbio za Mwenge wa Uhuru zikianza wilayani Shinyanga kwa kukagua miradi na kuweka jiwe la msingi.
Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru Luten Josephine Mwambashi, akikagua ujenzi wa Maabara ya Sayansi katika shule ya Sekondari Mwalukwa.
Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru Luten Josephine Mwambashi, akiweka Jiwe la Msingi katika Zahanati ya Bushushu.
Muonekano wa Jengo la Zahanati ya Bushushu.
Kiongozi wa Mbio Maalum wa Mwenge wa Uhuru Luteni Josephine Mwambashi, akiweka Jiwe la Msingi katika Nyumba za Watumishi mkoani Shinyanga zilizopo Negezi Manispaa ya Shinyanga.
Muonekano wa nyumba za watumishi.
Kiongozi wa Mbio Maalum wa Mwenge wa Uhuru Luten Josephine Mwambashi, akiweka jiwe la msingi katika Jengo la Uthibiti ubora wa Shule Kanda ya Magharibi.
Muonekano wa Jengo la Uthibiti ubora wa Shule Kanda ya Magharibi.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vija na Ajira, akifungua maji katika mradi wa maji Masekelo wa mtandao wa Ziwa Victoria ambao ulitembelewa na Mwenge wa Uhuru kuona maendeleo yake ya utoaji huduma kwa wananchi.
Koplo Rehema Ali Haji ambaye ni Miongoni mwa viongozi wa Mbio Maalum wa Mwenge wa Uhuru, akimtwisha ndoo ya Maji Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, kwenye mradi huo wa maji wa Masekelo unotekelezwa na Mamlaka ya maji na usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA.)
Ukaguzi wa mfumo wa TEHAMA katika Shule ya Sekondari Uhuru ukiendelea na viongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Awali Mkuu wa wilaya ya Shinyanga kushoto Jasinta Mboneko, akiwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Luteni Josephine Mwambashi katikati wakiendelea na ukaguzi wa miradi.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger