Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh.Dk.Philip Mpango (wa pili kutoka kulia) akipita katika banda la Barrick wakati alipotembelea maonesho ya Sabasaba.
Kampuni ya madini ya Barrick, inashiriki katika maonesho ya 45 ya kimataifa ya Biashara (SabaSaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam, ambapo banda lake la maonesho linaendelea kutembelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na wananchi ambao wanapata fursa ya kuelewa kwa undani shughuli za kampuni hiyo.
Mbali na ushiriki kampuni ya Barrick, pia imewezesha wajasiriamali kutoka vijiji vinavyozunguka mgodi wa Bulyanhulu uliopo mkoani Shinyanga, kwa ajili ya kuonesha bidhaa zao kwa lengo la kupata masoko zaidi na kupata maarifa kutoka kwa wajasiriamali wengine wanaoshiriki kwenye maonesho hayo.
Barrick imekuwa ikiwezesha wajasiriamali hao kwa kuwapatia elimu ya ukuzaji biashara zao, na kwa wale wanaoshughulika na kilimo wamekuwa wakipatiwa mbegu bora na mbolea.
Waziri wa Madini, Mh.Doto Biteko, akipatiwa maelezo ya shughuli za kampuni ya Barrick, kutoka wa wafanyakazi wa kampuni hiyo alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonyesho ya Sabasaba
Waziri wa Madini, Mh.Doto Biteko, akipatiwa maelezo ya shughuli za kampuni ya Barrick, kutoka wa wafanyakazi wa kampuni hiyo alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonyesho ya Sabasab
Waziri wa Madini, Mh.Doto Biteko, akipatiwa maelezo ya shughuli za kampuni ya Barrick, kutoka wa wafanyakazi wa kampuni hiyo alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonyesho ya Sabasab
Wafanyakazi wa Barrick katika banda la wajasiriamali kutoka Bulynhulu wanaoshiriki maonyesho ya biashara ya SabaSaba kwa ufadhili wa kampuni hiyo.
0 comments:
Post a Comment