Friday, 9 July 2021

BENKI YA CRDB YATOA MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI WA MADARASA KWA SHULE ZA SEKONDARI NA MSINGI WILAYANI KILINDI

...

 
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa kulia akimkabidhi mabati 360 yenye thamani ya Milioni 10 Mbunge wa Jimbo la Kilindi (CCM) Omari Kigua kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika sekta ya elimu kushoto anayeshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Kilindi Abel Busalama kulia ni Diwani wa Kata ya Mkindi Hillary Elisha Msigwa

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa kulia akimkabidhi mabati 360 yenye thamani ya Milioni 10 MKUU wa wilaya ya Kilindi Abel Busalama kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika sekta ya elimu kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Kilindi (CCM) Omari Kigua kulia ni Diwani wa Kata ya Mkindi Hillary Elisha Msigwa


MKUU wa wilaya ya Kilindi Abel Busalama akizungumza wakati wa halfa hiyo kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa na Mbunge wa Jimbo la Kilindi (CCM) Omari Kigua
MENEJA wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa akizungumza kabla ya makabidhiano hayo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kilindi Abel Busalama na Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Kilindi (CCM) Omari Kigua akifuatiwa na Diwani wa Kaya ya Mkindi Hilary Elisha
MBUNGE wa Jimbo la Kilindi (CCM) Omari Kigua akizungumza wakati wa Halfa hiyo kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa
MWALIMU Mkuu wa Shule ya Sekondari Mkindi Chiku Athumani akizungumza kabla ya halfa ya makabidhiano hayo


NA OSCAR ASSENGA, KILINDI.

BENKI ya CRDB imetoa msaada wa vifaa vya ujenzi wa Madarasa katika shule za Sekondari na Msingi wilayani Kilindi Mkoani Tanga wenye thamani ya Milioni 10 ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali kusaidia kuondoa changamoto zilizopo kwenye sekta ya elimu.

Vifaa hivyo vya ujenzi ambayo walikabidhi benki hiyo ni mabati 360 ambayo yalikabidhiwa kwenye Kata ya Mkindi wilayani humo ikiwa ni juhudi za Mbunge wa Jimbo la Kilindi (CCM) Omari Kigua kuwasilisha ombi lake kwa benki hiyo kuhusu uwepo wa changamoto hiyo.

Katika mabati hayo shule ya Sekondari Mkindi walipatiwa mabati 168 ambayo yatasaidia kupaua maadarasa yote, Kilindi Sekondari mabati 52,na Shule ya Msingi Masagusa mabati 50, Shule ya Msingi Michungwani mabati 50.

Akizungumza wakati wa halfa ya makabidhiano hayo Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa alisema kwamba benki hiyo inachukulia kwa uzito sana suala la uwekezaji kwenye sekta ya elimu.

Alisema kwamba hiyo imepekelea wao kama benki kuipa kipaumbele sekta ya elimu kupitia sera yao ya misaada ili kuunga mkono juhudi za wananchi na kurudisha kwao ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa na hamasa ya kutenegeneza miundombinu ya elimu kwa manufaa ya sasa na kizazi cha baadae.

“Benki yetu inajivunia kuona Taifa linapiga hatua kubwa kwenye sekta ya elimu ambapo kupitia sera ya serikali elimu bure imeongeza idadi ya wanafunzi lakini pia ufaulu ambao maendeleo yake yanaakiisi hadi kiwango chetu cha uchumi ambapo mwaka jana nchi iliingia kwenye uchumi wa kati”Alisema

Alisema katika jithiada za benki ya katika kuhamaisha elimu vilevile zinaokenaka katika kutekeleza sera ya benki katika kusaidia jamii ambayo inaelekeza kila mwaka asilimia 1 ya faida inayopatikana wanatakiwa kusaidia jamii kwenye Nyanja za elimu, afya na mazingira.

“Changamoto hizo ni pamoja na ukosefu wa mabweni, madarasa ya kutosha, umbali wa shule moja mpaka nyengine na vifaa vya kusomea jambo ambalo limekuwa likiathiri upatikanaji wa elimu kwa watoto”Alisema

Aidha alisema kupitia msaada huo ni matarajio yake kuwa utasaidia kuweka mazingira salama ya elimu kwa watoto 343 na hiyo itawezesha kujenga viongozi mahiri watakaokuja kuliongoza Taifa letu katika siku zijazo.

“Tunataka kuona wakina mama Samia Suluhu ,Tulia Akson,Ummy Mwalimu,Anna Makinda,Asha Rose Migiro na wengi zaidi katika nchi yetu”Alisema

Awali akizungumza kabla ya kupokea msaada huo, Mbunge wa Jimbo la Kilindi (CCM) Omari Kigua alisema anaishukuru CRDB kwa kuwaunga mkono kwenye sekta ya elimu kwa kuwapelekea mabati ambayo yatasaidia kuondosha changamoto zilizopo.

“Kilindi tunamshukuru sana Mkurugenzi wa CRDB kwa hayo yaliyoyafanywa katika wilaya hiyo yeye kama Mbunge, Mkuu wa wilaya na Mkugenzi wa Halmashauri watakuwa mabalozi wazuri sambamba na kwenda kuisemea benki hiyo “Alisema

Aidha alimuomba Meneja wa Kanda ya Kaskazini kuona namna ya kuwasaidia kuwachimbia kisima cha maji katika shule hiyo kutokana na kwamba wanataabika sana kusaka huduma hiyo muhimu.

“Katika hili tunakuomba umpelekee ombi kwa Mkurugenzi wa Benki ya CRDB kwamba tusaidiwe kutuchimbia kisima cha maji katika shule hii “Alisema

Hata hivyo Mkuu wa wilaya ya Kilindi Abel Busalama aliwataka walimu kuhakikisha mabati hayo yanatumika kwenye malengo yaliyokusudiwa na watakaotumia tofauti na malengo hayo watakuchukuliwa hatua..

“Ndugu zangu nikwaambie leo hii tunapokea msaada huu wa mabati kutoka Benki ya CRDB tusikute mabati haya mtaani …tutawachukulia hatua kali za kisheria wote ambao watabainika kuhusika”Alisema DC Abel.

Naye kwa upande wake Mkuu wa shule ya Sekondari Mkindi Chiku Athumani aliishukuru Benki ya CRDB kwa msaada huo ambao wameutoa ambao utasaidia kuondoa changamoto walizokuwa wakikabiliana nazo za uhaba wa vyumba vya madarasa.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger