Tuesday, 6 April 2021

RAIS SAMIA AAGIZA VYOMBO VYA HABARI VILIVYOFUNGIWA TANZANIA VIFUNGULIWE

...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
**
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameagiza kufunguliwa mara moja kwa kwa vyombo vya habari vilivyofungwana kusimamiwa ili vifuate sheria miongozo na kanuni.

Rais Samia ametoa agizo hilo leo Jumanne Aprili 6,2021 wakati akiwaapisha Makatibu Wakuu, Manaibu Makatibu Wakuu wa Wizara na Wakuu wa taasisi na Idara mbalimbali Ikulu Jijini Dar es salaam.

Amesema siyo vyema kutumia mabavu (nguvu) katika kuchukua hatua za kufunga vyombo vya habari.

"Naskia kuna Vi Tv  vya mkononi mmevifungia, vifungulieni. Vyombo vya habari mlivyovifungia mvifungulie na wafuate sheria, tusifungie tu kibabe, wafungulieni lakini tuhakikishe wanafuata miongozo na kanuni za serikali," amesema.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger