Picha ya msanii Peter Msechu akiwa na mkewe aliyembeba mtoto wao
***
Msanii wa BongoFleva Peter Msechu amenyoosha maelezo kwa baadhi ya watu wanaomshambulia mitandaoni kuhusu muonekano wake kwa kusema hawezi kubadilika na hiyo ndiyo brand yake pia haimuathiri kwa chochote.
Kupitia EATV & EA Radio Digital Peter Msechu amesema "Hakuna kitu kinachoniathiri nitabakia kuwa Msechu na brand yangu itabaki hivi hivi na nitaendelea kuishi maisha yangu na kuzingatia kula vizuri, kuishi vizuri, kufanya mazoezi na sina magonjwa nyemelezi"
"Kuishi kama shabiki yangu anavyotaka yeye ili afurahi sitaweza ila shabiki ndiyo apende maisha yangu, kitakachoniuma ni watoto wangu wakishinda njaa, kukosa ada au familia yangu kutokuwa vizuri, napenda na nafurahi watu wafanye hivyo kwa sababu inafanya nizidi kuzungumziwa wala hainiumi" ameongeza Peter Msechu
Aidha msanii huyo amesema Mungu amemuumba kila mtu kwa mfano wake na aina yake ambayo anataka ayaishi hapa duniani.
Chanzo - EATV
0 comments:
Post a Comment