Adela Ngogolo (42) amefungua kesi ya madai mahakama ya mwanzo Ilala akiomba kupewa talaka na mumewe, Alcado Mkondola (62) kwa madai kuwa ameshindwa kumpatiwa haki yake ya tendo la ndoa kwa miaka mitano mfululizo.
Mwanamke huyo anayeishi na mumewe Tabata Kimanga jijini Dar es Salaam ameieleza mahakama hiyo leo Jumanne Aprili 6, 2021 kuwa Mkondola hataki kushiriki tendo la ndoa kwa muda wa miaka mitano na kila akijaribu kumuomba unyumba anasukumwa na kuambiwa akalale chumba cha watoto.
Kesi hiyo ya madai namba 6/2021 aliifunguliwa mahakamani hapo Februari 25, 2021 na inasikilizwa hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Benjamin Mwakasonda.
Mwanamke huyo amedai mahakamani hapo kuwa kutoshiriki tendo hilo kwa muda mrefu kumesababisha apate madhara mbalimbali ikiwemo kuugua fangasi sehemu za siri kutokana na kujiingizia vitu visivyofaa ili kutuliza hamu.
Chanzo - Mwananchi
0 comments:
Post a Comment