Na WAMJW- Dom
Mganga Mkuu wa Serikali ametakiwa kusimamia mifumo ya uwajibikaji katika sekta ya afya nchini ili kupunguza vifo vya wajawazito pamoja na kupanua huduma za kibingwa ikiwemo vifaa vya kisasa ili kuvutia nchi za jirani kupata huduma za afya hapa nchini
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu Afya), Prof. Abel Makubi, tarehe 9 Aprili,2021 wakati akimkabidhi ofisi Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifelo Sichalwe kwenye ofisi ya Mganga Mkuu wa Serikali iliyopo katika mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.
Prof. Makubi ambaye alihudhumu nafasi ya Mganga Mkuu wa Serikali hapo awali amempongezà Dkt. Sichalwe kwa kuaminiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na kuteuliwa kuwa Mganga Mkuu wa Serikali.
Aidha, Prof. Makubi amemtaka CMO huyo kusimamia kusimamia suala la dawa, vifaa na vifaa tiba, kupambana na magonjwa yasiyoambukiza, huduma za tiba asili, ujenzi wa miundombinu pamoja na kusimamia mwenendo wa kuanza kwa Bima ya Afya kwa wote.
0 comments:
Post a Comment