Tuesday 2 March 2021

WAZIRI AWESO : MSIFANYE KAZI KWA MAZOEA, BADILIKENI KIFIKRA

...

Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza na wafanyakazi walio chini ya Wizara hiyo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Bonde la Kati mjini Singida
Wafanyakazi wa Bonde la Kati, Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Singida Mjini (SUWASA) na Wakala wa Usambazaji maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wakiwa kwenye mazunguzo na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Singida Mjini (SUWASA), Patrick Nzamba akimkaribisha Waziri wa Maji, Jumaa Aweso aweze kuzungumza na Wafanyakazi
****

 

Na Abby Nkungu, Singida
WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amewataka wafanyakazi wa Wizara hiyo kubadilika kifikra kwa kuanza kuchapa kazi kwa nguvu zaidi badala ya kuendelea kufanya kazi kwa mazoea.

Alitoa rai hiyo mjini Singida wakati akiongea na wafanyakazi wa Bonde la Kati, Mamlaka ya maji safi na Usafi wa mazingira Singida mjini (SUWASA) pamoja na Wakala wa usambazaji maji na Usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Singida.

Waziri Aweso alisema kuwa kwa kipindi kirefu sasa, Wizara hiyo imekuwa ikinyooshewa vidole kutokana na baadhi ya watumishi wake kukosa uaminifu na uadilifu; hivyo kushindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo.

"Yaliyopita si ndwele, tugange yaliyopo na yajayo. Ili kutimiza azma ya kumtua mama ndoo kichwani, lazima kila mfanyakazi aondokane na uvivu, afanye kazi kwa kutumia taaluma yake na kwa kuiheshimu taaluma hiyo naamini fedha nyingi zitolewazo na Serikali zitatumika vizuri kwa manufaa ya wananchi" alisema na kuongeza;

Hii itarejesha heshima ya Wizara yetu.....Nataka zikitajwa Wizara tatu zinazofanya kazi vizuri, sisi Wizara ya Maji tuwemo".

Alisema kuwa kutokana na ukweli kwamba maji hayahitaji porojo, ngojangoja wala hakuna mbadala wake, wafanyakazi wote wa Wizara hiyo hawana budi kushikamana na kufanya kazi kwa pamoja kwa kuwa wote ni familia moja.

"Ili tuijenge Wizara yetu tushikamane, tujiepushe na majungu na fitina lakini pia pale mnapofanya kazi nzuri ionesheni na kuitangaza kwa umma ili mtambulike".

Adha, alitoa mwito kwa Menejimenti zote kuhakiksha zinajali maslahi ya wafanyakazi wake kwa kuwa maslahi duni humnyong'onyesha mtumishi lakini maslahi bora humtia nguvu na kumjaza ari ya kufanya kazi zaidi.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger