Monday 29 March 2021

BENKI YA CRDB YATOA ZAWADI KWA RPC MAGILIGIMBA, DC MBONEKO WANAWAKE MASHUJAA SHINYANGA

...

Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Bw. Luther Mneney akimkabidhi zawadi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba (kulia) ikiwa ni sehemu ya pongezi za Benki ya CRDB tawi la Shinyanga kutambua mchango wake katika mkoa wa Shinyanga na kumpongeza kushinda tuzo ya Mwanamke Kinara katika uongozi taasisi za umma Kanda ya Ziwa.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Benki ya CRDB tawi la Shinyanga imetoa zawadi kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko ili kutambua mchango wao katika jamii na serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi.

Zawadi hizo zimekabidhiwa na Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Bw. Luther Mneney leo Jumatatu Machi 29,2021 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika benki ya CRDB.

"Leo Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga tumefika katika ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba kwa ajili ya kumpongeza kwa kazi nzuri anayofanya katika mkoa wetu pamoja kumpongeza kwa kushinda Tuzo ya Mwanamke Kinara Kanda ya Ziwa upande wa viongozi wa taasisi za umma",amesema Mneney.

Mneney ameongeza kuwa Benki ya CRDB inajivunia kiongozi Mwanamke ambaye ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba kwani imeona shughuli anazozifanya na waliomchagua kupata tuzo hawakukosea na anastahili kupata tuzo hivyo benki inampongeza kwa hilo na kumtakia kila la heri.

Pia ,Meneja huyo wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga amefika katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe.Jasinta Mboneko kwa ajili ya kupeleka salamu za Benki ya CRDB na kumkabidhi zawadi ya kutambua uwezo wake kama kiongozi shujaa kwenye wilaya ya Shinyanga.

“Benki ya CRDB tulikuwa na maadhimisho ya wiki ya wanawake duniani ambayo mwaka huu tumeitumia kuwatambua wanawake na shughuli wanazifanya na michango yao kwa jamii

Mhe. DC Tumefika hapa ofisini kwako kwani Benki ya CRDB inakujali na kuthamini mchango wako kwa jamii kama mwanamke shujaa na kupitia kwako tunataka kuhamasisha wanawake wengine watambue kuwa wana uwezo kama wanaume wasikae nyuma, wakae mbele taifa na dunia inawatambua. Wanawake wala hawahitaji kuwezeshwa kwani Mungu alipowaumba tu akawapa uwezo wa kuongoza”,ameongeza Mneney.

Akipokea zawadi hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba ameishukuru Benki ya CRDB kwa kuona na kutambua uwezo wake katika uongozi.

“Nichukue nafasi kuishukuru Benki ya CRDB namna mlivyoona ni vyema kufika katika ofisi hii kunipa pongezi za mimi kupata tuzo ya mwanamke kinara uongozi taasisi za umma. Nimefurahi kuona mmetambua hilo na kwamba mmekuja kunikabidhi zawadi hapa.

“Nawashukuru sana CRDB, niseme tu kwamba tuzo hii imenipa chachu ya kufanya kazi na nitaendelea kuchapa kazi na nimeamini kuwa kazi tulizozifanya jamii au taasisi za umma na binafsi wanaona kazi tunazofanya nikaona na mimi jina langu nikashinda tuzo”,alisema Kamanda Magiligimba.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko aliishukuru Benki CRDB kwa kutambua mchango wake katika shughuli za kijamii na kiserikali pamoja na kwenye Benki ya CRD kwani yeye ni miongoni mwa wadau wa benki hiyo.

“Niwapongeze CRDB kwa namna mnavyoendelea kuhudumia wananchi wa wilaya ya Shinyanga na muendelee hivyo hivyo kuwa ‘Active’ na kuendelea kushughulikia masuala ya maendeleo ya wananchi na kutangaza fursa za kusaidia wanawake ikiwa ni pamoja na kupunguza riba ya mikopo kwa wanawake na kuboresha zaidi huduma kwa wateja, kushughulikia malalamiko mnayoletewa huku mkiendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona”,amesema Mboneko.

Mkuu huyo wa wilaya amesema serikali itaendelea kushirikiana na Benki hiyo katika kuwaletea maendeleo wananchi.

Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Bw. Luther Mneney akimkabidhi zawadi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba (kulia) ikiwa ni sehemu ya pongezi za Benki ya CRDB tawi la Shinyanga kutambua mchango wake katika mkoa wa Shinyanga na kumpongeza kushinda tuzo ya Mwanamke Kinara katika uongozi taasisi za umma Kanda ya Ziwa leo Jumatatu Machi 29,2021 katika ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Bw. Luther Mneney akimkabidhi zawadi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba (kulia) ikiwa ni sehemu ya pongezi za Benki ya CRDB tawi la Shinyanga kutambua mchango wake katika mkoa wa Shinyanga na kumpongeza kushinda tuzo ya Mwanamke Kinara katika uongozi taasisi za umma Kanda ya Ziwa. Kushoto ni Meneja Huduma kwa Wateja Benki ya CRDB tawi la Shinyanga George Nyegu.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Bw. Luther Mneney akimkabidhi zawadi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba (kulia) ikiwa ni sehemu ya pongezi za Benki ya CRDB tawi la Shinyanga kutambua mchango wake katika mkoa wa Shinyanga na kumpongeza kushinda tuzo ya Mwanamke Kinara katika uongozi taasisi za umma Kanda ya Ziwa leo Jumatatu Machi 29,2021 katika ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Bw. Luther Mneney akimkabidhi zawadi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba (kulia) ikiwa ni sehemu ya pongezi za Benki ya CRDB tawi la Shinyanga kutambua mchango wake katika mkoa wa Shinyanga na kumpongeza kushinda tuzo ya Mwanamke Kinara katika uongozi taasisi za umma Kanda ya Ziwa 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba (kulia) akiishukuru Benki ya CRDB tawi la Shinyanga kutambua mchango wake katika maendeleo ya mkoa wa Shinyanga na kumpongeza kushinda tuzo ya Mwanamke Kinara katika uongozi taasisi za umma Kanda ya Ziwa 
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Bw. Luther Mneney (kulia) akimkabidhi zawadi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Zawadi kutoka Benki ya CRDB ikiwa ni sehemu ya kutambua uwezo wake kama kiongozi shujaa kwenye wilaya ya Shinyanga.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Bw. Luther Mneney (kulia) akimkabidhi zawadi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Zawadi kutoka Benki ya CRDB ikiwa ni sehemu ya kutambua uwezo wake kama kiongozi shujaa kwenye wilaya ya Shinyanga.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Bw. Luther Mneney (kulia) akizungumza baada ya kumkabidhi zawadi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Zawadi kutoka Benki ya CRDB ikiwa ni sehemu ya kutambua uwezo wake kama kiongozi shujaa kwenye wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza baada ya kupokea zawadi kutoka Benki ya CRDB ikiwa ni sehemu ya kutambua uwezo wake kama kiongozi shujaa kwenye wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza baada ya kupokea zawadi kutoka Benki ya CRDB ikiwa ni sehemu ya kutambua uwezo wake kama kiongozi shujaa kwenye wilaya ya Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger