Monday, 1 March 2021

WAHARIRI WASHUHUDIA UJENZI WA MRADI WA BWAWA LA NYERERE (JNHPP) UNAOENDELEA USIKU NA MCHANA

...

Kaimu Mhandisi Mkazi wa ujenzi wa Bwawa la Julius Nyerere Hydro Power Project (JNHPP) Lutenganya Kamugenyi akiwaelezea Wahariri wa vyombo mbalimbali hatua inayoendelea sasa katika Bwawa la Kuzalisha Umeme (Main Dam) ambapo amesema hatua inayoendelea sasa ni kujenga ukuta wa Zege wa bwawa hilo unaotarajiwa kukamilika mwezi Novemba Mwaka huu ili kupisha zoezi la Uvunaji Maji yatakayotumika kuzalisha umeme wa Megawati 2115. Ziara hiyo ya Wanahabari imefanyika Februari 28 , 2021 na imeandaliwa na Shirika la Umeme Tanzania( TANESCO).
Meneja Uhusiano TANESCO Johari Kachwamba akizungumzia umuhimu wa ziara hiyo ya wahariri wa vyombo vya habari katika Bwawa la JNHPP.

...................................................

Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wametembelea mradi mkubwa wa kimkakati wa bwawa la kufua umeme wa maji la Julius Nyerere Hydro Power Project (JNHPP-2115) lililoko bonde la mto Rufiji na kujionea ujenzi ukiendelea kwa kasi usiku na mchana katika maeneo yote muhimu matano.

Wahariri hao wametembeela eneo la ujenzi wa bwawa (Main Dam), eneo la kuchepusha maji (Diversion Tunnel), eneo la (Power Intake) na eneo la kufua umeme (Power Generation).

Lakini pia wahariri hao wametembelea maeneo mengine ya ujenzi kama vile eneo la kuchukulia umeme (Switch Yard) na sehemu ya mitambo ya kuchanganya zege.

Wahariri wa wameonyesha kufurahishwa na ziara hiyo ambapo kwa nyakati tofauti wamepongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa uamuzi wake wa kutekeleza mradi huo kwa gharama za watanzania wenyewe kwa sababu hii ilikuwa ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Akielezea utekelezaji wa mradi huo Kaimu Mhandisi Mkazi wa ujenzi wa Bwawa la Julius Nyerere Hydro Power Project (JNHPP) Lutenganya Kamugenyi amesema ujenzi wa mradi huo unaendelea usiku na mchana ambapo pia tahadhari zote zinazoweza kukwamisha shughuli za ujenzi zimechukuliwa hata mvua ikinyesha ujenzi utaendelea kama kawaida.


Kaimu Mhandisi Mkazi wa ujenzi wa Bwawa la Julius Nyerere Hydro Power Project (JNHPP) Lutenganya Kamugenyi akiwaelezea wahariri eneo la ujenzi wa sehemu ya kuchota umeme unaotoka kwenye mashine za kkufua umeme (Tibines) (Switch Yard) tayari umeanza
Ujenzi wa Eneo la Power House patakapofungwa mitambo 9 ya kufua umeme unavyendelea.
Wahariri wakiendelea na ziara katika eneo la Power House.
Baadhi ya mafundi wakiendelea na kazi.
Hili ndilo eneo ambalo limechepushwa maji ili kupisha ujenzi wa tuta kubwa (Main Dam) uendelee.

Kaimu Mhandisi Mkazi wa ujenzi wa Bwawa la Julius Nyerere Hydro Power Project (JNHPP) akilielezea eneo la kuchukulia maji ya kufua umeme Power Intake lenye matundu matatu makubwa yatakayotoa matundu matatu kila moja na kufikisha matundu 9 yatakayofungwa mitambo 9 ya kufua umeme.
Hili ni eneo la kuchukulia maji ya kufua umeme Power Intake lenye matundu matatu yatakayotoa matundu matatu kila moja na kufikisha matundu 9 yatakayofungwa mitambo 9 ya kufua umeme.
Wahariri wakitembelea eneo la mradi huku mitambo mikubwa ikiwa kiwa kazini
Wahariri wakiendelea na ziara kwenye ujenzi wa Bwawa la JNHPP.
Wahariri wakishuhudia kazi ya ujenzi wa tuta kubwa ukiendelea.
Wahariri wakitembelea eneo la ujenzi wa Power House.
Eneo litakalokuwa na Matundu 9 ya kupitishia maji kuingia kwenye mitambo ya kufua umeme. Kutakuwa na jumla ya mitambo tisa (Tibines) ya kufua umeme.
Picha ya Pamoja
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger