Sunday, 21 March 2021

MWILI WA MAGUFULI WAZUNGUSHWA UWANJA WA TAIFA MARA TANO BAADA YA ZOEZI LA KUAGA KUSITISHWA

...

Baada ya shughuli ya kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli kusitishwa katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam kutokana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza, mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe alitangaza utaratibu wa kuaga mwili kwa kuuzungusha uwanjani hapo.

Mwili huo ulipakiwa kwenye gari maalum lililokuwa na maofisa wa jeshi na kuzungushwa katika uwanja huo mara tano ikiwa ni baada ya maelfu ya wananchi kuulizwa wanataka uzungushwe mara ngapi.

“Wananchi mwili utazunguka uwanja ukiwa kwenye gari mara tatu, kila mmoja pale alipo apunge mkono, tufanye kama bungeni wanaokubali mara tatu waseme ndiyo,” amesema Gondwe lakini wananchi walikaa kimya.

Mkuu huyo wa Wilaya akauliza tena, “wanaosema hapana,” na wananchi wakajibu, “hapana” lakini aliposema mwili wa kiongozi huyo uzungushwe mara tano ili wamuage wananchi hao walisema kwa sauti, “ndio.”

Kuanzia saa 9:23 alasiri gari lenye mwili huo lilianza kuzunguka uwanja huo huku mamia ya wananchi wakipunga mkono na wengi kuonekana wakifuta machozi. Msafara ulizunguka uwanja huo hadi saa 10:10 jioni na kuanza safari ya kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ajili ya safari ya Dodoma.

 Via Mwananchi

UPDATES ZOTE

Pakua / Download App ya Malunde 1 blog Tuwe tunakutumia taarifa zote moja kwa moja kwenye simu yako bure kabisa 

Bofya <<HAPA>> Mara Moja Tu



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger