Finland imetajwa kuwa mahali pa furaha zaidi ulimwenguni kwa mwaka wa nne mfululizo, katika ripoti ya kila mwaka iliyofadhiliwa na Umoja wa Mataifa. Ripoti ya Furaha ya Ulimwenguni imeiweka Denmark katika nafasi ya pili, kisha Uswizi, Iceland na Uholanzi.
New Zealand ilikuwa tena nchi pekee isiyokuwa ya Ulaya katika 10 bora.
Uingereza ilishuka kutoka nafasi ya 13 hadi 17.
Takwimu kutoka kwa kampuni ya utafiti ya Gallup aliwauliza watu katika nchi 149 kukadiria furaha yao wenyewe.Vipimo vikiwa ni pamoja na usaidizi wa kijamii, uhuru wa kibinafsi, pato la taifa na viwango vya rushwa pia vilijumuishwa katika utafiti huo.
Nchi iliyoonekana kuwa isiyo na furaha zaidi ulimwenguni ilikuwa Afghanistan, ikifuatiwa na Lesotho, Botswana, Rwanda na Zimbabwe.
Kulikuwa na "kiasi cha juu cha hisia sizizokuwa nzuri" katika zaidi ya theluthi moja ya nchi, wachapishaji wa ripoti walisema, labda wakionesha athari za janga hilo.
Walakini, mambo yalikuwa mazuri kwa nchi 22. Nchi kadhaa za Asia zimefaulu kupiga hatua nzuri kuliko ilivyokuwa katika viwango vya mwaka jana, huku Uchina ikisonga juu hadi nafasi ya 84 kutoka 94.
"Cha kushangaza hakukuwa na, kwa ujumla kupungua kwa ustawi wakati unapokadiriwa na tathmini ya watu wenyewe ya maisha yao," John Helliwell, mmoja wa waandishi wa ripoti hiyo, alisema katika taarifa.
"ufafanuzi mmoja ni kwamba watu wanaona Covid-19 kama tishio la kawaida, la nje linaloathiri kila mtu na kwamba hii imesababisha hali kubwa ya mshikamano na hisia za kupambana pamoja ."
Finland "iliorodheshwa juu sana kwa hatua za kuaminiana ambazo zimesaidia kulinda maisha na jinsi watu wanavyokimu maisha yao wakati wa janga hilo", waandishi walisema.
Mataifa ya Denmark, Finland, Iceland, Norway na Sweden, pamoja na manaeo yake kama vile (Greenland, visiwa vya Faroe na Ă…land Island) yaliyo na idadi ya watu milioni 5.5 yamekabiliana vyema na hali hii kuliko nchi nyingi za Ulaya na zaidi ya visa 70,000 vya Corona na vifo 805, kulingana na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.
New Zealand ilishika hadi nafasi ya tisa, na ilikuwa nchi pekee isiyokuwa ya Ulaya iliyoorodheshwa katik 10 bora
Kulingana na ripoti hiyo nchi zilizo na watu wenye furaha ni:
Finland
Denmark
Uswizi
Iceland
Uholanzi
Norway
Sweden
Luxembourg
New Zealand
Austria
0 comments:
Post a Comment