Mwili wa aliyekuwa Rais wa awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli ulipowasili jijini Dodoma na kupokelewa na maelfu ya wananchi. Shughuli za kuaga mwili wa marehemu Dkt. John Pombe Magufuli Kitaifa ni tarehe leo 22 Machi, 2021 katika Uwanja wa Jamhuri ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan atawaongoza viongozi kutoka mataifa mbalimbali na wananchi katika kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu.
Pakua / Download App ya Malunde 1 blog Tuwe tunakutumia taarifa zote moja kwa moja kwenye simu yako bure kabisa
0 comments:
Post a Comment