Wednesday 3 March 2021

MWALIMU AMKATA PANGA MWALIMU MWENZAKE OFISINI WAKIGOMBANIA PENZI LA MWANAFUNZI WA 'FIELD'

...
Picha haihusiani na habari hapa chini
*
Polisi katika Kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya wamemkamata mwalimu wa Shule ya Upili ya Wasichana ya Karoti baada ya kudaiwa kumshambulia mwenzake kwa panga wakiwa afisini. 

Kamanda wa polisi Mwea Mashariki Daniel Katavi alisema mshukiwa huyo anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Wang’uru.

"Pia tumepata silaha ambayo inasemekana alitumia kumshambulia mwenzake katika eneo la shule," Kitavi aliiambia Citizen Digital.

 Kulingana na mkuu huyo wa polisi, mtuhumiwa alimshambulia mwenzake wa kiume kuhusu madai ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwalimu mwenzao wa kike ambaye yuko katika mazoezi ya kufunza shuleni humo. 

"Walimu hao wawili wa kiume wako kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwalimu mmoja wa kike ambaye yuko Field shuleni hapo, ”Kitavu alisema.

Mkuu huyo wa Mwea Mashariki alisema mtuhumiwa alidhani alikuwa amemuua mwenzake.

 "Alikuwa bado angali shuleni baada ya tukio hilo wakati wenzake walikuwa wakihangaika kumsaidia mwathiriwa na wengine wakiwaita maafisa wa polisi. 

Atashtakiwa kwa jaribio la mauaji, ” Kitavi aliongeza. Mhasiriwa, Alfose Orina anasemekana kuwa katika hali mbaya katika hospitali ya kibinafsi huko Mwea baada ya kukatwakatwa kichwani. 

Tukio hilo linajiri wakati Wizara ya Elimu inakabiliana na kuongezeka kwa visa vya utundu katika taasisi za elimu.

Waziri wa Elimu George Magoha alisema kuwa visa vya wanafunzi kuwashambulia walimu na utumiaji wa dawa za kulevya viliongezeka baada ya shule kufunguliwa Jumatatu, Januari 4.

 Wanafunzi katika taasisi mbali mbali kote nchini waliripotiwa kuchoma mabweni, kuwashambulia walimu na wanafunzi wenzao wakitumia silaha hatari.

Kuhusiana na kisa cha hivi punde kuwahusu walimu hao haijabainika iwapo Tume ya Huduma ya Walimu (TSC) itachukua hatua dhidi ya mwalimu huyo.

Chanzo- Tuko News

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger