Monday 1 March 2021

MBUNGE ANENGUA KIUNO LIVE MBELE YA WANANCHI AKICHEZA NGOMA YA DIAMOND PLATNUMZ

...

Mbunge Aisha Jumwa aliwatumbuiza wananchi wakati wa kampeni za UDA eneo la Matungu baada ya kunengua kiuno akicheza wimbo maarufu wa Diamond, Waah 
Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa aliwanengulia wakazi wa Matungu kiuno.
**
Mbunge wa Malindi nchini Kenya Aisha Jumwa amewachangamsha wakazi wa Matungu baada ya kunengua kiuno chake akicheza wimbo wa Diamond Platnumz wa Waah wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo ujao.

Jumwa alikuwa anampigia debe mgombea wa United Democratic Alliance (UDA) Alex Lanya ambapo alimuomba DJ kumchezea wimbo wa Diamond wa Waah ili kuwathibitishia wakazi ana kipaji cha kutingisha kiuno.

Punde wimbo huo maarufu ulipopasua anga, mwanasiasa huyo mashuhuri alianza kutingisha kiuno chake na kuwafurahisha wakazi.

Huku akiwa amezamishwa na muziki, baadhi ya wakazi walijiunga pamoja naye kwenye jukwaa na kumsaidia kuwatumbuiza wenzao ambao walishindwa kuficha furaha yao Jumwa akisakata ngoma.

 Uchaguzi Mdogo wa Machi 4,202.

Katika hotuba yake, mwanasiasa huyo wa Tanga Tanga aliwaomba wakazi kumpigia kura mgombea wa UDA, Lanya katika uchaguzi mdogo wa Machi 4 ambapo atamenyana na wagombea wengine 15. 

Alisema viongozi wa Magharibi kama vile Musalia Mudavadi na Francis Atwoli wamekuwa wakiwapoteza wakazi wa eneo hilo kwa muda mrefu.

 "Siku hiyo ya uchaguzi, ninawaomba nyinyi nyote mumpigie kura Lanya ili tuweze kurejea tena kuanza safari ya kuingia Ikulu pamoja," alisema.

Kama ilivyoripotiwa awali, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) iliwaidhinisha wagombea 15 kuwania kiti hicho ambacho kilisalia kufuatia kifo cha Justus Murunga. Wagombea hao ni ikiwemo Bernard Wakoli, Gregory Atoko, Kevin Nectus, Wilberforce Lutta, Athman Wangara, Anzelimo Kongoti na Samuel Munyekenye. Wengine ni Peter Nabulindo (ANC), David Were (ODM), Alex Lanya (UDA), Charles Kasamani (UDP), Paul Achayo (MDG) na Faida Auma wa Maendeleo Chap Chap.

Chanzo - Tuko News

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger