MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akiwahutubia wananchi wa kata ya Maweni Jijini Tanga wakati wa mkutano wake wa kampeni |
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akiwahutubia wananchi wa kata ya Maweni Jijini Tanga wakati wa mkutano wake wa kampeni |
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba akizungumza kwenye mkutano huo ambapo aliwataka wananchi hao kumchagua Ummy Mwalimu |
KATIBU Mwenezi wa CCM wilaya ya Tanga Lupaskiyo Kapange akimuombea kura Ummy Mwalimu wakati wa mkutano huo |
Mwenyekiti Mstaafu wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Tanga (UVCCM) Abdi Makange |
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kushoto akimnadi mgombea Udiwani wa Kata ya Maweni (CCM) Joseph Calvas wakati wa mkutano huo |
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ameahidi kumaliza tatizo la migogoro ya ardhi katika kata ya Maweni Jijini Tanga endapo akichaguliwa kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Octoba mwaka huu kwa kuhakikisha wananchi wanapata haki.
Ummy ambaye ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto aliyasema hayo wakati wa mkutano wake kampeni uliofanyika mtaa wa Kange Kata ya Maweni Jijini Tanga.
Aliwataka wampe mamlaka ya kuwa mwakilishi wao ili kuweza kukomesha migogoro hiyo kwa kuhakikisha wananchi wanapata haki ikiwemo wale waliopo kwenye maeneo yenye migogoro wanafanyiwa urasimishaji kwa bei inayoshikika na sio beii kubwa.
“Nipeni mamlaka ya kuwa mwakilishi wenu,nipeni mmlaka ya kuwa msemaji wenu,mamlaka ya kuwa kiongozi wenu migogoro ya ardhi tutaikomesha katika kata ya Maweni hususani kuhakikisha wananchi wanapata haki “Alisema
“Ikiwemo wananchi waliipo kwenye maeneo yaliyo kuwa na mgogoro eneo la Jaribu tena pamoja na maeneo ya Kasera wanafanyiwa urasimishaji kwa bei inayoshikika na sio bei kubwa hili nalibeba wana Maweni naombeni mniamini mnitume nikawatumikie”Alisema
Akizungumzia kwa upande wa sekta ya Afya ,Ummy alisema kwamba sekta hiyo kwenye nchi hii ni moja ya sekta iliyopata mafanikio makubwa kwenye nchi yetu ikiwemo kwenye Jiji la Tanga.
“Nafahamu hatujajenga zahanati na vituo vya afya kwenye baadhi ya kata na maeneo yetu lakini tumehaidi kwenye ilani endapo mtanichagua mimi na Rais Dkt John Magufuli tutajenga miundombinu ya kutoa huduma za afya"Alisema
" Ikiwemo zahanati na vituo vya afya katika maeneo kwa kuzingatia Geografia na eneo husika idadi ya watu pamoja na mzigo wa magonjwa kwa hiyo nikipita tutakaa na diwani tupange vipaumbele wapi tuweke zahanati wapi tujenge kituo cha Afya”Alisema
Alisema kazi kubwa imefanyika katika utoaji wa huduma za afya na kubwa ambalo bado hatujakamilishwa ni kuhakikisha wananchi wengi wanajiunga na bima ya afya ili waweze kupata huduma za matibabu bila kikwazo cha fedha.
“Kwenye hili naomba mniamini ni jambo kubwa ambalo Rais Magufuli amedhamiria kulitekeleza kwa miaka mitano inayokuja kuhakikisha wana Maweni,wana Tanga ,Watanzania wanapata bima ya Afya kubwa ili kuweza kupata huduma bora za Afya bila kikwazo cha fedha”Alisema
Alisema pia amedhamiri kuleta mapinduzi ya kweli ya kiuchumi na kijamii katika Jiji la Tanga hivyo wampe heshima ya kuwa mbunge wao ili aweze kuchochea kasi ya ukuaji wa maeneo kwao na jamii zinazowazunguka.
Awali akizungumza wakati wa kampeni hizo Mwenyekiti Mstaafu wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Tanga (UVCCM) Abdi Makange alisema baada ya Ummy Mwalimu kabla ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa viti maalumu mkoa wa Tanga katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo wakina mama walikuwa wakijifungua watoto njiti watatu lazima mmoja anakufa kutokana na kukosekana kwa vifaa.
Alisema kutokana na uwepo wa tatizo hilo walilazimika kumfuata Ummy Mwalimu akawapelekea vifaa ambavyo vimekuwa mwarobaini mkubwa wa kumaliza tatizo hilo na hivi sasa hakuna mtoto njiti anayefariki kwenye hospitali hiyo.
0 comments:
Post a Comment