Tuesday, 29 September 2020

WAZIRI UMMY ATOA AGIZO KWA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI NCHINI

...
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto akizungumza na wananchi wa Kata ya Pongwe Jijini Tanga wakati wa mkutano wake wa kampeni
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akimnadi mgombea udiwani wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kata ya Pongwe Jijini Tanga
MWENYEKITI wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba akimuombea kura mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katikati akiwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba wakitembea kwenye maeneo mbalimbali Pongwe wakati wa kampeni ya mgombea ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu
MSANII Kasim Mganga akitumbuiza wakati wa kampeni hizo
Umati Mkubwa wa wananachi wakifuatilia kampeni hizo
Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Tanga Lupakisyo Kapenge kulia akiwa na wadau mbalimbali wakifuatilia mkutano huo

 

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka wakurugenzi wa Halmashauri kote nchini kuacha kuwapa wanawake mikopo kiduchu ambayo haiwezi kuwasogeza mbele kimaendeleo.

 

Badala yake amewataka wawape mikopo itakayowawezesha kuwasaidia kufanya shughuli zao ambazo zinaweza kubadilisha maisha yao na hivyo kujikwamua kiuchumi wao na jamii zao

 

Ummy ambaye pia ni Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) aliyasema hayo wakati akizungumza na wananch wa Kata ya Pongwe Jijini Tanga wakati wa mkutano wake wa hadhara ambapo alisema katika hili amedhamiri kuhakikisha linafanyiwa kazi.

 

“Ninajua Katika hili ninaongea kama Waziri ninayesimamia Maendeleo ya wanawake ninawataka wakurugenzi kote nchini kuacha kuwapa wanawake mikopo ya laki tano, laki mbili, milioni moja badala yake wawapeni ya milioni 5, 10 na 20 ili muweze kufanya shughuli ambazo zinaweza kubadilisha maisha yenu na sio kuwadanganya na mikopo kiduchu ambayo haiwezi kuwasogeza mbele”Alisema

 

Alisema katika ilani ya uchaguzi ya CCM wamehaidi kwamba endapo watakichagua chama cha Mapinduzi (CCM) na endapo watamchagua wataongeza idadi ya wanawake watakaopata mikopo bila riba ili waweze kufanya shughuli zao na ujasiriamali.

 

“Ninawaomba sana wanawake wa Kata ya Pongwe ninafahamu hapa kwenu kuna vikundi 7 vimepata mikopo lakini vingi havijapata mikopo ninawaomba sana katika hili mniamini nitashirikiana na Diwani tuwafikie wanawake wengi zaidi hivyo ninaomba mnichague suala hili nikalisimamie kikamilifu”Alisema Waziri Ummy.

 

Katika ilani hiyo hawajawashau wafanyabiashara na wajasiramali wadogo wadogo huku akiwaomba wakiamini chama cha Mapinduzi (CCM) wamchague Rais Joh Magufuli na yeye ili waweze kuweka mazingira mazuri zaidi ya kwa wafanyabsiuara wadogo wadogo, wajasiramali wadogo wakiwemo mama ntilie wauza ngenge na vijana wa bodaboda waweze kufanya shughuli zao bila vikwazo.

 

“Lakini pia ninatambua hapa Pongwe kuna matatizo ya upatikanaji wa maji bado maeneo ya Kakindu,Kisimatui na Kilango na hili limeanza kuonekana baada ya maji kupelekwa Muheza hapa kwetu Pongwe upatikani wa maji umekuwa changamoto niwaombe mniamini nitalifanyia kazi”Alisema

 

Ummy alisema kwamba tayari alikwisha kuanza kulifanya kazi suala hilo na Tanga Uwasa tayari wamekwisha kupata fedha za kuboresha mtandao wa maji  ili kuweza kuongeza idadi ya kaya na nyumba ambazo zinapata maji safi na salama ili kuhakikisha maji yanapatikana kwenye eneo hilo kwa muda mrefu.

 

Mwisho.

 

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger