Polisi jijini Nairobi nchini Kenya wanafanya uchunguzi ambapo mwanamke aitwaye Jesca Sibwe mwenye umri wa miaka 42 ambaye amefariki dunia baada ya kulala Lojing'i 'gesti' usiku kucha na shemeji yake aitwaye John Kisongona Mareko.
Inasemekana marehemu Jesca Sibwe ambaye anatoka Kasarani alianza kuugua ghafla kabla ya kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Kenyatta.
Kulingana na ripoti ya polisi, Jesca alialikwa na ndugu wa kiume wa mumewe John Mareko kwenye hoteli ya Graceland maeneo ya Dubois siku ya Jumatano, Septemba 23,2020.
Mareko alikuwa amewasili saa moja kutoka Malindi ambapo wawili hao walilala katika hoteli ya Graceland.
Inaelezwa kuwa Mwanamke huyo alianza kukohoa na ndiposa wakaitisha teksi ya kumkimbiza KNH ambapo madaktari walithibistisha tayari alikuwa amekata roho
Mwili wake ulipelekwa katika makafani ya hospitali hiyo kusubiri upasuaji huku maafisa kutoka Idara ya Upelelezi wakianzisha uchunguzi kuhusiana na kisa hicho.
Mwezi Juni 23, kisa sawia na hicho kililiripotiwa katika hoteli ya Amazon mjini Kakamega kuwahusu jamaa na mrembo ambaye ilisemekana ni mpenziwe.
Kamanda wa kituo cha Kakamega ya kati David Kabena alisema Manala aliwasili katika gesti hiyo akiwa ameandamana na dada aliyetambulika kama Anyango.
"Wawili hao waliagiza waletewe chajio kabla ya kuingia hoteli ya Amazon. Ni dada pekee tu alikula chakula," polisi walisema.
Rekodi zilionyesha kwamba dada huyo mwenye umri wa miaka 31 aliwasili mjini humo mchana ambapo waliandamana hotelini humo na kulipa ambapo walilala usiku huo.
Hata hiyo, mambo yalibadilika baada ya mrembo kugundua jamaa alikuwa ameaga dunia ghafla wakati asubuhi ilipofika.
Inasemekana marehemu alikuwa na mke na watoto.
Chanzo - Tuko news
0 comments:
Post a Comment