Mgombea urais wa CHADEMA, Tundu Lissu, ameahidi kufanya mabadiliko ya kiuchumi na kiutawala kama atachaguliwa.
Akizungumza na mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Mwanga mjini Kigoma, aliwataka Watanzania kupiga kura kwa CHADEMA, ili kufikia mabadiliko makubwa ya maisha yao .
"Kama mgombea wa CHADEMA katika jimbo hili ana nguvu mchagueni huyo na kama mgombea wa Chama cha ACT-Wazalendo ana nguvu muungeni mkono, yeyote mwenye nguvu ndio mgombea wangu," alifafanua katika jimbo hilo ambalo mgombea wa ACT-Wazalendo ni Zitto Kabwe.
Lissu alisema iwapo atashinda urais wa Tanzania, atakuwa wa tofauti , kwa kuwa atafanya mabadiliko ya mfumo wa utawala kupitia mabadiliko ya Katiba inayoendana na mazingira ya sasa ya nchi.
Kwa mujibu wa Lissu, ili atekeleze majukumu yake ameaahidi kufanya mabadiliko ya katiba kwa kupeleka muswada wa mabadiliko bungeni ndani ya siku 100 za kwanza baada ya kuapishwa kwake.
0 comments:
Post a Comment