Sunday, 13 September 2020

Raia 7 wa Kigeni Watiwa Mbaroni Kwa Wizi wa Mtandaoni

...
Jeshi la Polisi limekamata raia saba wa kigeni kwa kosa la wizi wa mitandaoni. Watuhumiwa hao raia wa Nigeria, Liberia, DRC, India na Afrika Kusini wenye umri kati ya miaka 28 na 44 walikamatwa kati ya mwezi Agosti na Septemba mwaka huu.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam SACP Lazaro Mambosasa, amesema watuhumiwa hao wamekiri kujipatia kiasi cha shilingi milioni kumi (Tsh 10,000,000/=) kihalifu, na kutumia pesa hizo kufungua duka la pombe kali, kununua gari aina ya MARK II, runinga mbili na magodoro.

Aidha, Mambosasa amesema wapo katika msako wa kuwatafuta Watanzania walioshirikiana na wahalifu hao. Na kuwataka wageni wote wanaoingia nchini kwetu kufuata sheria zilizopo.

Watuhumiwa wote bado wanashikiliwa na polisi na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger