Thursday, 3 September 2020

MAMIA WAJITOKEZA UZINDUZI KAMPENI ZA UCHAGUZI CCM KATA YA BAKOBA BUKOBA

...
Mgombea udiwani kata Bakoba akiwaomba wananchi Kura akiwa amepiga magoti chini ndugu Shabani Said

Na Ashura Jumapili - Bukoba

Mamia ya wananchi wa Kata Bakoba iliyopo Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera,wamejitokeza katika ufunguzi wa kampeni za uchaguzi katika Kata hiyo ulioandaliwa na Chama Cha Mapinduzi kata hiyo.


 Mgombea udiwani Kata ya Bakoba kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM )Shabani Saidi ,alinadi sera zake mbalimbali ikiwemo kusaidia kupunguza umbali wa  watoto wa wanasoma chekechea na awali wanaotembea umbali wa zaidi ya kilimota moja kwenda shule ya msingi Bunena wakitokea mtaa wa Kafuti.

Saidi alisema ipo haja ya kujengwa kwa shule ya chekechea na awali katika maeneo licha ya ombi Hilo kuombwa na wananchi wa maeneo husika pia miundombinu ya barabara ya maeneo hayo ya Bunena kwenda Kalobela sio rafiki kwa watoto hao wenye umri mdogo.

Mgombea huyo  kitaaluma ni Mwalimu  na ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Bukoba mjini  mwaka 2017/2022.

Alisema amewiwa kugombea katika nafasi hiyo ili aweze kuhamasisha jamii kuwekeza katika elimu ili kuongeza ufaulu kupitia kambi za wanafunzi.

Alisema pia atashiriki katika ujenzi wa shule kwaajili ya watahiniwa wanao hitimu kidato Cha nne kuweza kujiunga na kidato Cha tano katika shule ya kata itakayokuwepo.

Alisema hoja nyingine ni kuhusu mikopo ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kuwa atawasaidia wajasiriamali wadogo kujiunga na vikundi ili waweze kupata fursa hiyo ya mikopo kwa madai kuwa wajasiriamali walio wengi hawajui jinsi gani fedha hizo za serikali zinapatika Tena kwa masharti nafuu.

Alisema kupitia mikopo hiyo wataweza kukuza mitaji yao na kupanua wigo wa biashara zao na kuinua kipato kwa ngazi ya familia sanjari na kuondokana na umasikini katika jamii.

Alisema wananchi wa Kata hiyo wanayo fursa kubwa ya kufanya biashara kupitia bandari ya Bukoba, na viwanda mbalimbali vilivyopo katika Kata hiyo Kama vile kiwanda Cha kusindika na kukoboa Kahawa ( TANICA ),Kiwanda Cha kukoboa Kahawa ( BUKOP ) na kiwanda Cha maji.

Alisema pia Kuna changamoto ya miundombinu mibovu ya barabara za mitaa zilizopo katika Kata hiyo ambazo zinaweza kutengenezwa hata kwa kutumia nguvu za wananchi wakati serikali ikiendelea kujipanga kuzitengeneza wao watakuwa wamepigwa hatua kubwa.

Alisema hoja ya nne ni maboresho ya zahati ya kata hasa kuongeza jengo mama na mtoto kutokana na ongezeko la watu kwa madai kuwa lililopo halitoshelezi mahitaji ya watu wa eneno husika.

Alisema pia atasimamia katika suala la Ajira katika viwanda vilivyopo katika Kata hiyo Wazawa wenye sifa wanapewa kipaumbele.

Alisema atasimamia sheria kanuni na taratibu za uwekezaji katika kata hiyo iliyobarikwa kuwa na viwanda mbalimbali ikiwemo Wazawa wenye sifa kupewa kipau mbele kwenye soko la Ajira

Mgombea huyo aliwaomba wananchi wa kata hiyo kuchagua mafiga matatu kwa maendeleo yao ambayo ni diwani ,mbunge na Rais wote wa Chama Cha Mapinduzi.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria uzinduzi wa kampeni hizo za Kata Bakoba





Said Shabani mgombea udiwani kata Bakoba
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger