Saturday, 5 September 2020

CHADEMA WAZINDUA KWA KISHINDO KAMPENI TARIME VIJIJINI... HECHE ASEMA USHINDI LAZIMA

...
 Mgombea Ubunge jimbo la Tarime vijijini kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akiwatubia wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni zake uliofanyika uwanja wa Tarafa Sirari.

*****
Na Mwandishi wa Malunde 1 blog Tarime

Mgombea Ubunge Jimbo la Tarime Vijijini John Heche kupitia chama cha Democrasia na Maendeleo(CHADEMA)amezindua rasmi kampeni zake na kueleza mambo mbalimbali aliyotekeleza wakati akiwa mbunge huku akiwaomba wananchi kumchagua tena ili aendelee kuleta maendeleo.

Heche aliyasema hayo jana wakati akizindua kampeni katika uwanja wa Tarafa kijiji cha Sirari kata ya Sirari wilayalani Tarime,uzinduzi ambao uliohudhuriwa na viongozi wa chama hicho kutoka wilaya mbalimbali za mkoa wa Mara,wakiwemo wagombea Ubunge kupitia chama hicho pamoja na Wananchi.

Heche alisema kuwa iwapo kura hazitatosha atawashukuru wananchi na kwenda kufanya shughuli zake kwa sababu anaamini katika democrasia,lakini akishinda na akatangazwa mwingine atahakikisha anapambana ili haki ipatikane huku akiwaomba wananchi wamchague pamoja na Mgombea urais Tundu Lissu na madiwani wa CHADEMA.

Akizungumzia maendeleo yaliyofanyika Heche alisema kuwa miradi mbalimbali imetekelezwa katika awamu yake ya ubunge,ikiwemo miradi mbalimbali ya ujenzi wa Zahanati,Vituo vya Afya,HospitalI ya Halmashauri,Miundobinu ya Barabara,mikopo, na miradi mingineyo.

Aliongeza kuwa kutekelezwa kwa miradi hiyo ni kutokana na halmashauri hiyo kuongozwa na CHADEMA ambapo Madiwani walisimamia miradi vizuri na masuala mbalimbali ya maendeleo.

Baadhi ya wagombea ubunge kutoka majimbo mbalimbali mkoani Mara nao wakampigia kampeni mgombea huyo na kuwataka wananchi wampigie kura Heche.

Mgombea Ubunge jimbo la Bunda mjini Esther Bulaya kupitia chama hicho aliwaomba wananchi kumchagua Heche kwani ndiyo anazijua shida za Tarime hivyo atatatua kero za wananchi.

Mgombea Ubunge Jimbo la Tarime mjini Esther Matiko alisema Heche ni kiongozi mzuri hivyo kuwaomba wananchi wampe kura.

Mgombea Ubunge jimbo la Serengeti  Catherine Luge alisema kuwa amefanya kazi na John Heche anamfahamu katika utendaji wake wa kazi na amekuwa akitetea haki ya maslahi ya wananchi wa Tarime.

"Chadema imetoa wanawake watatu kutoka Mara kugombea ubunge sisi ni wasubhati (Mabinti)zenu tupeni kura mpeni John ili akamilishe mipango iliyosalia kwa maendeleo ya Tarime" alisema Luge.

Mgombea Ubunge jimbo la Musoma mjini Mwita Julius aliwaomba wananchi kuipigia kura Chadema kwa kuwa ni chama kinachotetea matatizo ya wananchi.

Mgombea Ubunge kutoka jimbo la Rorya Ezekiel Wenje alisema kuwa Heche ni mtu mwenye msimamo na amekuwa akifanya kazi nzuri akiwa bungeni na kwamba majimbo ya Tarime yamekuwa kimaendeleo ikilinganishwa na jimbo la Rorya.

"Shida tulizonazo Rorya nyie hamjui kwa miaka 20 mfululizo Rorya imeongozwa na CCM lakini iangalie  barabara zenyewe  ni shida,sisi ndiyo tuko karibu na ziwa lakini hatuna maji safi na salama  hatuna maji ya bomba  na uongozi ni wa CCM naombeni muipe Chadema kura",alisema Wenje.

Mzee maarufu kutoka kijiji cha Bisarwi kata ya Manga Marwa Kisang'ore alisema kuwa Serikali ya Tarime mwaka 2017 iliwafukuza wakulima wenye mashamba kandokando mwa mto Mara ili kupisha kilimo cha Sukari lakini John Heche alipambana kuhakikisha ardhi inarudi kwa wananchi.

"Heche ni mfuata nyayo mzuri Apiri,2,2017 tulifukuzwa kwenye ardhi  kuanzia huko Nyamongo,Nyawana,Weigita,Kiore,hadi kirumi Heche alitupigania na Serikali ikazuia ardhi yetu kuporwa,alitusemea bungeni na ardhi ikarudi mikononi mwetu kura zote tutampa Heche", alisema.

Katibu wa CHADEMA wilaya ya Tarime Hamis Nyanswi alisema"kuna watu wanaona Chadema imepoteza mwelekeo sisi hatujapoteza mwelekeo tuna sababu ya kuichagua Chadema kwa kuwa ni mwakilishi wa wananchi, watu wanasema ukiichagua Chadema maendeleo hayaji mbona Rorya haina maendeleo ikilinganishwa na majimbo ya upinzani japo imeongozwa na CCM ",alisema Nyanswi.

Mwenyekiti wa chama cha Democrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Mara Lucus Ngoto alisema kuwa katika kuhakikisha wanawake wanapata nafasi za uongozi kimeteua wanawake 3 kati ya majimbo 10 kugombea ubunge wa jimbo.
 Mgombea Ubunge jimbo la Tarime vijijini kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni zake uliofanyika uwanja wa Tarafa Sirari.
 Mgombea Ubunge jimbo la Tarime vijijini kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni zake uliofanyika uwanja wa Tarafa Sirari.
 Mgombea ubunge jimbo la Tarime kupitia chama  cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA Esther Matiko akimnadi mgombea ubunge jimbo la Tarime vijijini John Heche wakati wa uzinduzi wa kampeni za Heche
 Wagombea ubunge majimbo ya mkoa wa Mara kupitia CHADEMA wakiwa wenye uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge jimbo la Tarime vijijini John Heche
 Wafuasi wa CHADEMA na wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge jimbo la Tarime vijijini John Heche.
 Wagombea ubunge na wafuasi wa CHADEMA wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za John Heche mgombea ubunge jimbo la Tarime vijijini.


Mgombea ubunge jimbo la Bunda mjini kupitia CHADEMA Esther  Bulaya akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge jimbo la Tarime vijiji John Heche.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger