Thursday, 20 August 2020

HALMASHAURI KUU YA CCM MKOA WA TANGA YAWAPITISHA WAGOMBEA 245 NGAZI YA UDIWANI MKOA MZIMA

...

 

HALMASHAURI kuu CCM mkoa wa Tanga imewapitisha kwa kauli moja wagombea wote 245 walioomba kuwania nafasi ya udiwani katika wilaya zote nane mkoani hapo.

Hayo yalibainishwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga Shaibu Akwilombe wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kuwa katika kikao hicho cha Halmashauri kuu mkoa kilichofanyika Agosti 18 mwaka huu.

Alisema kikao hicho kiliamua kuwapitisha wagombea wote wa udiwani walioshika nafasi ya kwanza waliopitishwa katika kura za maoni na kwenye vikao husika vya kata wilaya kwa sababu kiliafikiana na maoni ya vikao hivyo .

Aidha alisema kwamba mkoa wa Tanga  una kata 245 zinazopatikana katika Halmshauri 11ambapo kila kata ilitoa mgombea aliyeshinda kwa nafasi ya kwanza.
 

Hata hivyo alisema kwamba katika mchakato huo hakuna aliyeshika nafasi ya pili na kupata fursa ya kuipeperusha bendera bali ni wale ambao walishinda kwenye kura za maoni ambao waliyepitishwa katika kikao hicho.

Alisema kuwa uamuzi huo umeweka rekodi ya kihistoria kwa wagombea wote waliopata nafasi ya kwanza kupitishwa katika kuwania nafasi hiyo ya udiwani.

Aliongeza kwamba wapo waliopata nafasi ya pili na ya tatu na kuendelea lakini hawakuweza kukidhi  vigezo
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger