Monday, 31 August 2020

Makonda Amshukuru Mungu Baada Ya Kupata Watoto Mapacha..."Niliitwa Tasa"

...
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  na mkewe, Maria,  wamepata watoto wengine wawili ambao ni mapacha wa kiume na wa kike.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Makonda amethibitisha kuwa mkewe Maria amejifungua na kufanya idadi ya watoto wao kufikia watatu sasa huku akimshukuru Mungu kwa zawadi hiyo kwani hapo awali aliitwa tasa lakini leo ameuona ukuu wa Mungu.

"Heshima na Mamlaka ni zako eee Mungu wa Mbingu na Nchi na kwako wewe tunalia Aba, nitaendelea kutaja ukuu wako siku zote za maisha yangu kwakua hujawahi kuniacha hata dakika moja.

"Pamoja na mapito magumu na mazito lakini naiona nuru yako huku nikisikia sauti ya ROHO mtakatifu ikisema mwanangu Paul Christian Makonda nalikujua kabla sijakuumba na nikakutenga kwa kusudi langu usikubali TAA iwakayo ndani yako ikazimika.

"Ona sasa unavyozidi kuniheshimisha katikati ya machozi umenipatia zawadi tena itokayo kwako.

"Mimi nilieitwa tasa ulinipa mtoto KEAGAN ambaye alishangaza ulimwengu kwa ujio wake: Ukaona haitoshi LEO umenipa DOUBLE PORTION:Leo Mungu wangu umenipa MAPACHA tena wa KIUME na Wa KIKE hii yote ni kutangaza UKUU wako maishani mwangu.

"Kwa wale ambao bado hawajakuamini na wanateseka juu ya uzazi,naomba kupitia watoto hawa wakauone ukuu wako Ewe YESU mwana wa Mungu ulie hai. Hongera sana kipenzi changu Maria Mungu amejitwalia utukufu kupitia wewe.

"Asanteni sana watumishi wa Mungu, wazazi wetu, dada na kaka zetu kwa kuwa nasi nyakati zote, kama ambavyo mmekuwa baraka kwetu.Naomba pia Mungu awainulie watu wema nyakati za uhitaji wenu.

#EhhNafsiYanguMUHIMIDI-Bwana
#MoyoWaShukrani,” ameandika Makonda.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger