Monday, 31 August 2020

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Akabidhi Ramani Ya Tanzania Inayoonyesha Afya Ya Udongo Kwa Taha

...
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Kusaya jana (30.08.2020) amefanya kikao na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Kuendeleza Mazao ya Bustani (TAHA) Dkt.Jacquline  Mkindi jijini Arusha cha kujadili mikakati na mambo mbalimbali yahusuyo maendeleo ya tasnia ya mboga mboga na matunda (horticulture) nchini.

Sambamba na kikao hicho, Katibu Mkuu Kusaya ameikabidhi TAHA zawadi ya Ramani ya Tanzania inayoonesha viwango vya pH na Afya ya Udongo kwa nchi nzima na imepokelewa na Mtendaji Mkuu wa TAHA, Dr. Jacqueline Mkindi.

Kusaya ameitaka TAHA kuendelea kuelimisha wakulima wengi zaidi kuzingatia kilimo cha kitaalam kwa kutambua aina ya udongo unaofaa kwa zao husika na mbolea gani itumike, ndio maana amekabidhi ramani hiyo kuwezesha utambuzi wa maeneo yanayofaa kwa mazao ya horticulture nchini.

“Tunaendelea kuishukuru Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa ushirikiano mkubwa na wa muda wote inaotupatia wadau wa sekta ya horticulture ” Dr Mkindi alisema.

Katibu Mkuu Kusaya alikuwa mkoani Arusha Kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kutembelea taasisi zinazojihusisha na kilimo vikiwemo viwanda vya kuzalisha mbolea kwa matumizi ya kilimo.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger