Thursday, 20 February 2020

WATU 8 WAUAWA KWA RISASI UJERUMANI

...

Mwanaume mmoja nchini Ujerumani amewaua kwa risasi watu wanane waliokuwa katika klabu mbili tofauti za shisha.

Matukio hayo yalitokea usiku wa kuamkia jana katika mji wa Hanau ulipo katika Jimbo la Hessen, Mashariki mwa jiji la Frankfurt.

Aidha, katika matukio hayo mwanaume huyo pia aliwajeruhi watu wengine watano.

Polisi nchini Ujerumani ilisema kuwa mwanaume huyo alitekeleza matukio hayo kwa nyakati tofauti kati ya saa saa 4.00 na 7.00 usiku.

Hata hivyo, mwanaume huyo alikutwa amekufa saa chache baada ya kutekeleza uharifu huo.

Wakizungumzia tukio hilo, polisi walisema mtuhumiwa huyo awali alivamia katika baa moja iliyopo katikati mwa jiji huo na kufyatua risasi ovyo zilizosababisha vifo vya watu watatu.

“Baadaye alikimbia na kwenda katika baa nyingine iliyopo katika kitongoji cha Hanau Kesselstadt na kuua watu wengine watano,” ilisema taarifa hiyo ya polisi.

Kwa mujibu wa polisi, haijajulikana sababu ya mauaji hayo na kwamba uchunguzi umeanza mara moja.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger