Saturday, 8 February 2020

Wananchi Mkoani Kagera Waweka Itikadi Zao Za Kisiasa Pembeni Na Kuanza Kuchapa Kazi Kwa Pamoja.

...
Na Avitus Benedicto Kyaruzi,Kagera.
Itikadi za kisiasa zimetajwa kama changamoto kubwa inayowakumba wananchi katika Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera kushindwa kuhudhuria vikao mbalimbali vya maendeleo ususani katika sekta ya maji.
 
Hayo yalibainishwa na Diwani wa kata ya Katoma Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera Mh Deusdelith Rwekaza  kupitia Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo (CHADEMA) mnamo tarehe 07/02/2020 katika kikao cha majumuisho ya kujadili rasimu ya taarifa ya ufatiriaji na uwajibikaji jamii katika setka ya maji katika halmashauri hiyo kikao kilichoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Faraja For Hope And Development Organization(FAHODE) .
 
Katika kikao hicho  ambacho kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa sekta ya maji akiwemo Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa halmashauri, Afsa maendeleo jamii mkoa pamoja na wilaya, Afisa mipango, Afisa Takukuru wilaya, Madiwa wa kata za Kemondo, Katelero,Ibwela,Katoma,Kemondo pamoja na Maruku, ambapo mradi huo wa maji unahudumu, Watendaji wa Kata pamoja na Vijiji na wadau mbalimbali wa maendeleo ususani katika sekta ya maji, kikao ambacho kilifanyikaa katika ukumbi wa mikutano wa Chemba uliopo katika halmashauri hiyo.
 
Katika kikao hicho diwani wa Kata ya Katoma mkoani Kagera Mh  Deusdelith Rwekaza alisema kuwa wananchi wa kata hiyo walikuwa wanahudhuria wachache katika vikao vya maendeleo ususani sekta ya maji  uku sababu ikitajwa kuwa ni itikadi za kisiasa jambo ambalo lilikuwa linarudisha nyuma ukamilishwaji wa miradi ya maji katika kata hiyo.
 
Katika kuhakikisha kwamba  wanamaliza tofauti zao mh Rwekaza alisema kuwa walikaa kikao cha pamoja huku wakimuusisha Mkuu wa Wilaya hiyo Mh Deodatus Kinawilo na wakaridhia kuweka pembeni itikadi hizo na kuwa kitu kimoja katika suala la maendeleo.
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali la Faraja For Hope And Development Organization(FAHODE) ameitaka jamii kufatilia kwa kina juu ya uwajibikaji pamoja na kutunza  vyanzo vya maji na kuviendeleza kwa ajili ya vizazi vilivyopo pamoja na vijavyo.
 
Aidha amewataka wananchi kuhoji miradi mbalimbali iliyopo kwenye kata zao ili kujua kwa kina kuhusu miradi hiyo uku akitumia nafasi hiyo kuipongeza timu iliyoundwa ili kutekeleza miradi ya maji ambayo iliweza kuzungukia miradi hiyo na kuweza kubaini changamoto mbalimbali zinazo ikabiri sekta hiyo ili kuweza kutafutiwa ufumbuzi.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger