Sunday, 16 February 2020

Wanafunzi waandamana kupinga adhabu shuleni

...
Wanafunzi wanaosoma Shule ya Sekondari Shinyanga (SHYBUSH), iliyopo wilayani Kishapu mkoani humo, wameandamana kwenda kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack wakilalamika kunyanyaswa na walimu, pamoja na kupewa adhabu zilizokithiri..

Kaka Mkuu wa shule hiyo Mwendesha Manyangu, akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake mara baada ya kufika kwa Mkuu wa Mkoa, alisema kumekuwa na malalamiko mengi ya wanafunzi kunyanyaswa na walimu shuleni hapo, pamoja na kupewa adhabu kwa makosa ambayo wangeonywa.

Alisema baada ya kilio hicho kuwa cha muda mrefu juu ya adhabu hizo wamekuwa wakimweleza Mkuu wa Shule hiyo Malambi Malelemba, lakini amekuwa hawajali na ndipo wakaamua kuandamana ili kipatiwe ufumbuzi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, aliwatoa wasiwasi wanafunzi hao na kubainisha kuwa malalamiko yao atayafanyia kazi, huku akiwawaonya kuacha kujiingiza kwenye migomo isiyo na maana ambayo inawapotezea muda wa masomo.

Pia aliwaonya wanafunzi ambao wamekuwa wahamasisha migomo shuleni, waache tabia hiyo mara moja, na kubainisha wale ambao wamehamasisha maandamano hayo watashughulikia ili liwe fundisho kwa wanafunzi wengine

Aidha Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Joseph Paul, aliwataka wanafunzi kuachana na makundi ambayo hayawajengi na kuanzisha migomo isiyo na faida, huku akishukuru hawakufanya fujo shuleni kwao ya kuharibu mali, na kuwasihi pale wanapokuwa na matatizo wafuate utaratibu. 


Credit: Nipashe 



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger