Tume ya Afya ya China imeripoti kuwa idadi ya vifo kutokana na virus vya Corona imefikia 2,004, huku idadi ya maambukizi ikiongezeka hadi 74,185. Hong Kong imeripoti kifo cha pili kutokana na maambukizi ya Virusi hivyo.
Ukraine imetangaza mpango wake wa kutuma ndege ili kuwaondoa Raia wake 49 waliopo nchini China.
Aidha, Mamlaka za Urusi zinazosimamia uthibiti wa Virusi ya Corona zimesema Raia wa China hawataruhusiwa kuingia nchini humo kuanzia Februari 20 2020. Wamesema zuio hilo ni la muda mfupi.
0 comments:
Post a Comment