Idadi ya maambikizi mapya ya virusi vya corona imepungua kidogo kutoka siku moja kabla.
Vifo vingine 97 na maambukizi mapya ya watu 3,062 vimeripotiwa katika muda wa masaa 24 yaliyopita jana Jumapili, ikilinganishwa na maambukizi mapya ya watu 3,399 yaliyorekodiwa siku moja kabla.
Wakati huo huo, timu ya wataalamu wa kimataifa kutoka shirika la afya ulimwenguni WHO imeondoka kwenda Beijing kufanya uchunguzi wa kuzuka kwa virusi vya corona, shirika hilo la afya la Umoja wa mataifa limetangaza.
Zaidi ya watu 40,000 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya corona duniani kote hadi leo Jumatatu asubuhi, ambapo watu 900 wamefariki.
-DW
0 comments:
Post a Comment