Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania (THBUB) imeeleza masikitiko yake kuhusu kauli zinazotolewa na baadhi ya viongozi na makundi ya kisiasa na kijamii zinazoashiria uvunjifu wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora nchini.
Kupitia tamko la tume hiyo lililotolewa jana Jumatano Februari 5, 2019 na mwenyekiti wake, Jaji mstaafu Mathew Mwaimu amesema kauli hizo zimekuwa zikichochea kwa kiasi kikubwa wananchi kujichukulia sheria mikononi kutokana na kutoridhishwa na vitendo vya baadhi ya wanasiasa.
Amesema hivi karibuni katika mitandao ya kijamii, watu wamekuwa wakitoa kauli za kuwatishia wenzao.
Ameeleza kuwa makundi mengine yamejitokeza kupinga hatua hiyo na kuahidi kuchukua hatua ambazo hazitoi sura nzuri katika ustawi wa misingi ya haki za binadamu na utawala bora nchini.
Ameeleza kuwa kauli hizo zisipodhibitiwa zinaweza kusababisha uvunjifu wa amani na utulivu uliopo nchini.
0 comments:
Post a Comment