Monday, 10 February 2020

Rais Magufuli Aresha Wanyamapori mbalimbali Ikulu Dar es salaam

...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amerejesha wanyamapori katika bustani za Ikulu Jijini Dar es Salaam hali iliyofanya mandhari ya Ikulu kupendeza na kuvutia.

Wanyama waliopo katika bustani hizo ni pamoja na Pundamilia, Pofu, Swala, Digidigi, Tausi, Mbuni, Tumbili, Kanga, Batamaji na wengine.

Awali wanyamapori hao walifugwa kwa idadi kubwa wakati wa Uongozi wa Awamu ya Kwanza chini ya Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na baadaye walitoweka hadi mwaka 2017 walipoanza kurejeshwa na Mhe. Rais Magufuli.

Katika maeneo ya Posta Jijini Dar es Salaam hivi sasa kuna ongezeko kubwa la ndege aina ya Tausi ambao wanaonekana kulipamba Jiji la Dar es Salaam.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger