Wednesday, 5 February 2020

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KATIBU MTENDAJI WA SADC, BALOZI WA EU NA BALOZI WA CHINA, IKULU DAR

...
Rais  Magufuli amekutana na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (Sadc), Dk Stergomena Tax, Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania, Manfred Fanti na Balozi wa China nchini humo, Wang Ke.


Baada ya mazungumzo yake leo Jumatano Februari 5, 2020 Ikulu ya Dar es Salaam, Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Sadc, Dk Tax amesema alikuja kutoa taarifa ya utekelezaji wa masuala mbalimbali ya jumuiya hiyo ikiwamo uendelezaji wa viwanda na kanda huru ya biashara ambapo wamekubaliana kuendelea kuhamasisha nchi wanachama kuendeleza viwanda ili kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi.

Ameelezea baadhi ya maeneo yaliyopo katika mkakati wa kukuza uchumi wa Sadc ni kuendeleza miundombinu hasa ya usafiri na nishati ambayo bado ni changamoto kwa nchi za Sadc lakini ameipongeza Tanzania kwa hatua madhubuti zinazoendelea kuchukuliwa ikiwamo ujenzi wa barabara, reli na kuongeza uzalishaji wa umeme.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger