Kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Francis jana alikataa pendekezo kutoka kwa maaskofu wa eneo la Amazon ambalo lingeruhusu watu waliooa kuwa mapadre na wanawake kuwa wahudumu wa kike kanisani, ili kujaza upungufu wa watu hao katika eneo hilo.
Jibu la Papa, lilikuwa linasubiriwa kwa hamu kubwa lakini alichagua kutohusisha suala la ndoa katika waraka wake wenye vipengee 111 chini ya kichwa cha habari Wapenzi Amazon.
Francis alitoa wito wa wamisionari zaidi kutumwa katika eneo la Amazon na kuwahimiza maaskofu wote kutoka Amerika ya kusini, kuwa wajitolea zaidi katika kuwahimiza wale ambao wanataka kwenda likizo ya umisionari kuamua kwenda katika eneo la Amazon.
Francis amelikwepa suala hilo kufuatia ukosoaji mkubwa kutoka kwa wahafidhina zaidi katika kanisa Katoliki.
Waraka wa hivi karibuni unaosisitiza maadili ya useja, ulioandikwa na kadinali robert Sarah, ulielezwa kuwa uliandikwa pia na Papa Emeritus Benedict wa 16.
0 comments:
Post a Comment