Wednesday, 5 February 2020

Palestina yakaribisha uungaji mkono wa EU na AU kukataa mpango wa amani wa Marekani kuhusu Mashariki ya Kati

...
Palestina imepongeza Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika kwa uungaji mkono wao kwa Palestina kukataa mpango wa Marekani kuhusu amani ya Mashariki ya Kati.

Waziri wa mambo ya nje wa Palestina Bw. Riyad al-Maliki amepongeza taarifa zilizotolewa na mwakilishi mwandamizi wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell na mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki ambazo wamekataa mpango wa Marekani.

Habari nyingine zinasema mwenyekiti wa baraza la utawala la Sudan Bw. Abdel Fattah al-Burhan amesisitiza tena msimamo wa Sudan kuiunga mkono Palestina na haki za watu wa Palestina kuanzisha nchi yao huru. 

Bw. Al-Burhan amesema hayo baada ya kukutana na waziri mkuu wa Israel Bw. Benjamin Netanyahu nchini Uganda.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger