Watu 26 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa nchini Thailand baada ya kupigwa risasi kiholela na mwanajeshi mmoja wa nchi hiyo katika mji wa Nakhon Ratchasima.
Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Thailand ameziambia duru za habari kwamba, Jakraphanath Thomma, afisa wa madaraka ya chini alimshambulia mkuu wake kabla ya kuiba bunduki na risasi kutoka katika kambi ya kijeshi.
Baadaye aliwafyatulia risasi waumini waliokuwa katika hekalu na duka la jumla katika mji huo.
Picha za vyombo vya habari zilionekana zikionyesha mshukiwa huyo akitoka katika gari moja katika eneo moja la duka hilo la jumla katika wilya ya Muang na kuwafyatulia watu risasi kiholela.
Picha nyengine zilionyesha moto nje ya jengo hilo, huku kukiwa na ripoti kwamba ulisababishwa na gesi iliolipuka baada ya kupigwa risasi .
"Mwanajeshi huyo alitumia bunduki ya rashasha kuwapiga risasi watu wasio na hatia na kuwajeruhi wengi huku wengine wakifariki''.
Msemaji wa idara ya ulinzi Luteni jenerali Kongcheep Tantravanich alisema kwamba watu zaidi ya 20 waliuawa.
Moja ya machapisho yake ya mitandao yanaonyesha picha ya selfie yake huku moto ukiwaka nyuma yake.
Ripoti zaidi zinasema kuwa, vikosi vya usalama vilimzingira mshambuliaji huyo na kumuua kwa kumpiga risasi.
0 comments:
Post a Comment