AFISA wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama Risasi Semasaba akimkabidhi fomu ya kuwania nafasi ya Uenyekiti wa Ngome ya Wanawake ACT Wazalendo Mkiwa Kimwanga
Mkiwa Kimwanga kushoto akijaza fomu kulia ni Afisa wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama Risasi Semasaba
Mkiwa Kimwanga akiwaonyesha fomu yake mara baada ya kukabidhiwa
NA MWANDISHI WETU,
MKIWA Kimwanga amechukua fomu za uenyekiti wa wa Ngome ya Wanawake Taifa ya Chama cha ACT Wazalendo.
Mkiwa ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Mkoa wa Mwanza amechukua fomu hizo mapema leo ikiwa ni Mwanamke wa Tatu kuchukua kujitokeza kuwania nafasi.
Wengine ambao wamekwisha kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo ni Janeth Rithe na Salma Mwasa ambapo uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Pazia la kuchukua na kurejesha fomu kwenye uchaguzi wa ACT Wazalendo unatarajiwa kufanyika mwezi Machi Mwaka 2020 na litafungwa February 26 mwaka huu
0 comments:
Post a Comment