Mwakilishi wa Misri katika Umoja wa Mataifa ametaka bara la Afrika lipewe viti viwili vya kudumu katika Baraza la Usalama la umoja huo na haki ya kura ya veto (turufu).
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imesema kuwa, mwakilishi wa nchi hiyo katika Umoja wa Mataifa, Mohamed Idris ametoa ombi hilo sambamba na kuanza kikao cha duru mpya ya mazungumzo ya Baraza la Usalama kuhusu mabadiliko na ustawi ndani ya jumuiya hiyo ya kimataifa.
Taarifa hiyo imesema kuwa, mwakilishi wa Misri katika UN ameashiria makubaliano yaliyofikiwa baina ya viongozi wa nchi za Afrika katika mkutano wa siku chache zilizopita mjini Addis Ababa chini ya uenyekiti wa Misri na kusisitiza kuwa: Cairo inataka bara la la Afrika lipewe viti viwili vya kudumu katika Baraza la Usalama na mamlaka kamili ikiwa ni pamoja na haki ya kura ya turufu.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lina jumla ya wanachama 15, na wanachama 5 miongoni mwao wana haki ya kutumia kura ya veto.
0 comments:
Post a Comment