Wednesday, 19 February 2020

Mbwa Koko Azua Balaa Uwanjani.....Mbwa huyo aliingia uwanjani na kumiliki mpira huku juhudi za kumpokonya mpira huo zikigonga mwamba

...
Video moja imetrend sana mtandaoni ikimuonyesha mbwa koko akisitisha mechi baada ya kuingia uwanjani na kuchukua umiliki wa mpira wakati wa mechi jijini Istanbul.

Katika Video hiyo fupi ya mnamo Jumatano, Februari 18, mbwa huyo mweupe anaonekana akikimbia uwanjani wakati wachezaji walikuwa wanajiandaa kuanza mechi.

Kisha mbwa huyo aliuchukua mpira na kuanza kucheza nao na kuwaduwaza wachezaji, refa na hata mashabiki.

Juhudi za wachezaji kujaribu kuchukua mpira huo zilionekana  kugonga mwamba.

Mchezaji mmoja alijaribu kupiga mpira huo nje ili kumfukuza mbwa huyo, lakini bado aliufuata na kurejea uwanjani.

Hatimaye mbwa huyo aliweza kuondolewa uwanjani na kupelekwa mahali salama na mmoja wa wachezaji kabla ya mechi hiyo kuendelea.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger